Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 1
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina swali moja tu la nyongeza. Tulikuwa na mpango wa ujenzi wa mabwawa mawili kwenye Wilaya ya Chemba, Bwawa la Ndoroboni na Bwawa la Babayu, naomba kujua sasa ujenzi wake utaanza lini? Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali moja la Mheshimiwa Monni, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kama Serikali tunatangaza jumla ya mabwawa 100 kwa ajili ya kufanya usanifu na kila usanifu unavyokamilika tutakuwa tunatangaza bwawa hilo katika mwaka huo wa fedha au mwaka mwingine wa fedha. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge, mimi na yeye tuonane baadaye tuangalie haya mabwawa mawili kama yamo ndani ya mabwawa 100 ambayo yametangazwa kwa ajili ya kufanyiwa usanifu. (Makofi)
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 2
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kuishukuru Serikali ya Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kiasi cha shilingi 3,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa skimu ambayo imeharibika zaidi ya miaka 40, Kijiji cha Nyamgogwa, Kata ya Shabaka, Wilaya ya Nyangh’wale. Je, ni lini Serikali itatangaza zabuni ya ujenzi wa skimu hiyo? Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Amar, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ukanda wa Lake Victoria kuanzia Mara, Simiyu, Geita na Mwanza sasa hivi wataalam wetu wanafanya kazi ya usanifu kwa ajili ya kuziangalia skimu na mabwawa ambayo yalishajengwa huko mwanzo na yakaharibika; na kwa kuwa, skimu hii ilipangwa kujengwa mwaka huu wa fedha, nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba usanifu ukikamilika tu itatangazwa kwa ajili ya kuanza kujengwa. (Makofi)
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 3
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi. Kwanza namshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupitishia bajeti ambayo inajenga mabwawa matatu; Bwawa la Ari, Bwawa la Dirim. Je, ni lini wametangaza mabwawa haya ili yaweze kujengwa na wananchi wa Mbulu Vijijini wapate kumwagilia mashamba yao? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni miongoni mwa mabwawa 100 ambayo yametangazwa katika Mkoa wa Manyara na nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa usanifu ukikamilika tu, mabwawa haya 100 ambayo yametangazwa sasa yataingia kwenye ujenzi. Tunatarajia usanifu utachukua kipindi cha miezi sita ili uweze kukamilika and then tuanze kutangaza mabwawa hayo. (Makofi)
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 4
MHE. NICODEMUS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuniwekea bajeti kwenye Skimu ya Isebya – Mgelele, lakini pia kuna Skimu nyingine iliyoko Bukombe mpakani Bugerenga ambayo tuna-share na Naibu Waziri Mkuu. Sasa ni lini Serikali itatoa pesa ili kusudi kazi ziende kufanyika? Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Maganga na ninamwomba kupitia Bunge lako Tukufu akubali mpango wa Serikali kutekeleza kwanza skimu hizi mbili za kwanza halafu na Jimbo la Bukombe tunazo skimu ambazo tunazitekeleza katika mwaka huu wa fedha. Tutaichukua skimu hii kuiingiza katika mpango wa mwaka ujao wa fedha. (Makofi)
Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 5
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza Skimu ya Umwagiliaji wa Bonde la Eyasi, Wilayani Karatu, wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 38 ambao hadi sasa utekelezaji wake unasuasua? Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kweli Eyasi kulitokea tatizo na msingi wa tatizo ulitokana na design ya awali, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali iko committed kuhakikisha kwamba tunajenga Skimu ya Eyasi na bwawa lake. Sasa hivi wameshafanya review ya design na mkandarasi atarudi site kwa ajili ya kuanza utekelezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Mbunge na Mbunge wa Karatu kwa jitihada alizozifanya kufuatilia changamoto zilizotokea katika ujenzi wa Skimu ya Eyasi, nimhakikishie kwamba mkandarasi atarudi site na kuendelea na ujenzi. (Makofi)
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 6
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naishukuru Serikali kwamba imeweka kwenye bajeti hii tunayoendelea nayo ujenzi wa Skimu ya Metrom, Makeresho na Bwawa la Bolutu. Ni lini sasa Serikali itaanza kujenga skimu hizi ambazo ni muhimu sana kwenye uzalishaji wa kilimo ndani ya Jimbo la Hai? Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli skimu mbili pamoja na bwawa zimeshatangazwa, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa taarifa nilizonazo mimi kama Waziri, tumeshatangaza Skimu ya Makeresho na hiyo nyingine itatangazwa muda si mrefu, Makeresho imeshatangazwa sasa hivi. (Makofi)
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 7
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Kasulu ipo Miradi ya Umwagiliaji katika Kata ya Titye na Rungwe Mpya. Miradi hiyo ilianza, lakini miundombinu yake haijakamilika kutokana na ukosefu wa pesa. Je, ni lini Serikali itapeleka pesa ili kukamilisha miradi hiyo? Ahsante.
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba tu nimjibu Mheshimiwa Genzabuke kwamba, nimezipokea hizi scheme mbili alizozitaja, nitaenda kuzifanyia kazi na nitampa majibu.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 8
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwamba, tunahitaji hizi scheme za umwagiliaji kwa manufaa makubwa, lakini hivi karibuni kumekuwa na matukio ambayo yanasababisha kuwapoteza ndugu zetu na hasa watoto. Imetokea kule Nzega, lakini na Rorya tulipoteza watoto sita. Sasa, nataka kujua mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba, miundombinu ya mabwawa haya inaboreshwa either kwa kuweka uzio ikiambatana na alama za kuonesha kwamba, ni eneo hatarishi ili tusiendelee kupoteza ndugu zetu ikiwepo sambamba na kujenga bwawa pembeni la kuchota maji au watoto wanavyoenda kwa recreation zozote zile? Ninakushukuru.
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka tu niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, mabwawa yote tunayojenga sasa hivi, tunayajengea fence, kwa maana ya kuwa na uzio wa kuzunguka katika maeneo yote. Mabwawa yote tunayoyajenga tunatengeneza spill over, kwa maana ya kwamba, maji yakijaa yanaenda kwenye bwawa dogo ambalo litakuwa linatumika vilevile, kwa ajili ya mifugo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, design ya mabwawa mengi sasahivi tunabadilisha, kwa ajili ya siyo tu kulinda usalama wa watu pekeyake, lakini vilevile kulinda usalama wa matuta ya yale mabwawa ili yaweze kuishi kwa muda mrefu.
Name
Justin Lazaro Nyamoga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza Skimu za Umwagiliaji katika Kijiji cha Takwa na Kidoka vilivyopo katika Jimbo la Chemba?
Supplementary Question 9
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nashukuru Wizara kuingiza kwenye bajeti Bwawa la Nyanzwa, kwa ajili ya umwagiliaji, lakini swali langu ni Scheme ya Ruaha Mbuyuni, bwawa lilibomoka muda mrefu na Mheshimiwa Waziri unafahamu. Ni lini sasa tutawasaidia wale wananchi kwa sababu, hali inazidi kuwa mbaya na mvua inakaribia? Nakushukuru.
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Kamonga kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Scheme ya Ruaha Mbuyuni kila mwaka imekuwa ikibomoka na kila wakati tumekuwa tukienda kufanya rehabilitation ndogondogo kufanya watu wafanye kazi. Kwa hiyo kama Wizara tumeamua tu kufanya usanifu wa kina, kwa ajili ya ile scheme yote na pale pana maji mengi, ili tuweze kuijenga complete, kama ambavyo tumefanya mkombozi badala ya kuendelea kupoteza fedha kufanya repair ndogondogo. Kwa hiyo, nawaomba wananchi wa eneo lile na wananchi wa Mkoa wa Iringa watuvumilie, usanifu unaendelea, ukikamilika tu itatangazwa, ili ijengwe properly tuondokane na hili tatizo la kujirudia kila wakati.