Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga jengo la Kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Muleba?

Supplementary Question 1

MHE. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na commitment ya Serikali kwamba jengo la Muleba litawekwa kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026. Wilaya ya Muleba ina majengo mengi ya Mahakama za Mwanzo ambayo yamechakaa. Je, Serikali ina mpango wowote wa kuyakarabati?

Mheshimiwa Spika, swali la pili: Kuna wadau walitupatia majengo kwa ajili kuyaendeleza kidogo na kuyafanyia ukarabati ili yatumike kama Mahakama za Mwanzo. Je, Serikali ililipokea hili jambo; na imepangia pesa kwa ajili ya kulikarabati ambalo liko Kata ya Ijumbi?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Mahakama nyingi kama nilivyosema kwenye jibu la msingi hazina hali nzuri. Ni kwa msingi huo ndiyo maana Idara ya Mahakama imeweka Mpango wa Miaka Mitano wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo haya. Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango huo unatekelezwa kadri ya upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, pia kwa taarifa, kwa ujumla Mahakama za Mwanzo ambazo zimejengwa na kukarabatiwa ni 185, Mahakama za Wilaya ni 66, Mahakama za Ngazi ya Mkoa ni saba na Mahakama Jumuishi ni zaidi ya 12. Kwa hiyo, mpango huu unatekelezwa kila mwaka. Itakapofikiwa Wilaya ya Muleba, pia itanufaika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, ni kwamba majengo tuliyapata kutoka kwa mdau; namwomba tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutawasiliana na Idara ya Mahakama wafanye assessment ya utoshelevu au kufaa kwa hilo jengo kuwa Mahakama ili ikiridhiwa, basi ukarabati ufanyike ili liweze kutumika kama Mahakama kwenye Kata ya Ijumbi, aliyoitaja. Nakushukuru.

Name

Aleksia Asia Kamguna

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga jengo la Kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Muleba?

Supplementary Question 2

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Morogoro Vijijini haina kabisa jengo la Mahakama. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga jengo la kisasa la Mahakama katika Halmashauri hiyo?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi, ni kwamba Wilaya zinaendelea kujengewa Mahakama kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa mpango wa Mahakama hivi sasa, Morogoro ina Wilaya tatu zilizopata ujenzi wa Mahakama. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kulingana na mahitaji, Wilaya ya Morogoro Mjini pia itafikiwa, nakushukuru.

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga jengo la Kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Muleba?

Supplementary Question 3

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Jengo la Mahakama ya Mwanzo Wilayani Urambo lina hali mbaya sana. Je, ni lini Serikali itatujengea jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, nikiri kwamba ni kweli nimeiona Mahakama ya Mwanzo Urambo, hadi picha nililetewa na tumethibitisha kwamba ni mbaya sana. Mahakama imeuweka ukarabati wa Mahakama ya Mwanzo Urambo katika bajeti ya mwaka 2025/2026, nakushukuru.