Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwantum Dau Haji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya Ugonjwa Sugu wa Kisukari nchini?
Supplementary Question 1
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza namshukuru Waziri kwa majibu yake mazuri aliyoyatoa hapo, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Je, kuzingatia ulaji unaofaa ni kupi?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili: Pamoja na nia njema ya Serikali kutoa elimu ya kutotumia pombe na tumbaku, kwa nini Serikali isiamue kuhamasisha matumizi ya pombe na tumbaku nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika,…
SPIKA: Ngoja kwanza, Mheshimiwa Mwantumu, ulikusudia kusema wahamasishe matumizi ya tumbaku na pombe ama ulikusudia wakataze?
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, wasitishe.
SPIKA: Wasitishe?
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, wasitishe kuhamasisha matumizi ya pombe na tumbaku nchini.
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza, namshukuru Mheshimiwa Mbunge, mama yangu, Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji kwa sababu amekuwa akifuatilia masuala ya afya, hata kule Muhimbili amekuwa akifuatilia wagonjwa mbalimbali ambao wanapata matatizo kama haya na kuhakikisha kwamba wanapata huduma, ahsante sana. Hata hivyo, nimwambie tu, amesema tufanye ulaji upi?
Mheshimiwa Spika, ili kuokoa muda, namwomba aende aka-google ahakikishe kwamba anasoma vizuri na kuzingatia maelezo ya mzee wangu Prof. Janabi. Kwa hiyo, ukienda pale, hayo yote anayoyasema Prof. Janabi tukiyazingatia tutaondokana na matatizo haya.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwenye suala la kusitisha pombe na sigara, kwa kweli mchakato umeanza, lakini utaona kwenye sigara na kwenye mambo mengine imehamasisha kwamba ina madhara kiafya. Sasa suala la kusitisha isitumike kabisa, ninachofikiri siyo kusitisha kabisa, nafikiri kila mtu atambue kwamba ukifanya jambo hili unapata madhara haya na ukiacha jambo hili unapata faida, na kila mtu azingatie hayo ambayo yanaelezwa na wataalamu wetu wa afya. Ahsante. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, swali lake la nyongeza la kwanza ameuliza hivi, “Ni ulaji upi unaofaa?” Sasa umemtuma Mbunge aende aka-google na akamfuatilie Prof. Janabi ambapo tuna maswali kwa kweli kwa yale anayohamasisha...
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika,…
SPIKA: Sasa kuna namna mbili; moja, labda useme utampatia Mheshimiwa Mbunge majibu ya ulaji unaofaa ni upi? Ama sivyo, nadhani lengo la Mbunge kuuliza hapa alikusudia Watanzania wapate picha ya ulaji unaofaa ni upi? (Makofi)
Sasa ninakupa nafasi wewe nenda ka-google, ukishaupata ule ulaji unaofaa utakuja hapa utupe hayo majibu kwa sababu mama wa watu yule hawezi kwenda ku-google. Kwa hiyo, nakupa nafasi Mheshimiwa. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kama utanipa nafasi mimi niliona tu kwamba nikianza kutumia muda kufafanua itachukua muda mrefu. Niseme kwamba kuna mambo rahisi, kwanza, kuhakikisha una uzito ule unaotakikana kulingana na urefu wako; uzito unaokubalika kwa maana ya kwamba ulaji wako unaweza ukala kila kitu, lakini kila jambo kwa kiwango, kupunguza wanga na vyakula vile vingine vinavyoongeza uzito, lakini kuhakikisha uzito wako uko kwenye kiwango na mafuta yaliyoko mwilini mwako yako kwenye kiwango ambacho hakina shida.
Mheshimiwa Spika, ndiyo maana nasema pia sisi binadamu tumezaliwa kwa natural kwenye genome yetu sisi kwa asili ni hunters and gatherers. Kwa maana hiyo, hakikisha vyakula ambavyo unakula vingi ni vile ambavyo vimetayarishwa, siyo fried foods. Ni vile vyakula vya asili kama mbogamboga. Ukila protini ziwe ni protini ambazo siyo fried. Kwa namna hiyo, tunaweza kuhakikisha kwamba afya yetu inakuwa nzuri.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni topic ndefu, ndiyo maana niliona nikianza kugagatua hapa itachukua muda mrefu sana. Kikubwa tuzingatie maelekezo ya wataalamu wetu, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved