Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Stella Ikupa Alex
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:- Je, hospitali ngapi zimetenga vyumba vya kujifungulia wanawake wenye ulemavu nchini?
Supplementary Question 1
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga vyumba hivi kwa sababu ni ombi ambalo nililitoa ndani ya Bunge lako Tukufu katika kipindi hiki cha miaka mitatu; lakini pia Mheshimiwa Rais alipotualika watu wenye ulemavu pale Ikulu alielekeza vyumba hivi vitengwe. Jibu la msingi limeonyesha mafanikio makubwa sana; kwa hiyo, ninamshukuru sana Mheshiwa Rais Dkt. Samia Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mafanikio haya makubwa, je, Serikali ina mpango gani sasa kuhakikisha kwamba vyumba hivi vinatengwa kwenye ngazi ya vituo vya afya pamoja na zahanati?
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nina ombi kwa Serikali. Katika hii shilingi bilioni 21.1 ambayo imetengwa kwa ajili ya kununua vifaatiba, basi iweze kuzingatia ununuzi wa zile adjustable beds ili ziweze kusaidia watu wenye ulemavu, wazee na wagonjwa ambao wanakuwa hawajiwezi. Ahsante.
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kulitazama hili eneo muhimu sana na amekuwa akifuatilia haya mambo kwa karibu. Nimwambie Mheshimiwa Mbunge, kwanza, moja tunaelekea kwenye dunia ya inclusion, kwa hivyo tusingependa kuona kwamba akina mama wanatengwa. Kwa sababu ukizungumzia akina mama wote ni akina mama, tofauti wana mahitaji tofauti. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa, kwenye vyumba vile vya kujifungulia tunaweka mazingira ambayo yanahakikisha mama mwenye ulemavu mahitaji yake yamezingatiwa, yatakayom-facilitate yeye aweze kujifungua kwa usalama na bila kupata shida yoyote. Pia, kujenga attitude ya watumishi wetu kuhakikisha anapokuja mama mwenye ulemavu basi wanapelekwa kulingana na anavyokuwa, kwa sababu hata walemavu wenyewe wana mahitaji tofauti tofauti wanapokuja kwenye eneo la kutibiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili la shilingi bilioni 21.1 ambazo zimetengwa na Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba zizingatiwe. Kwanza nimhakikishie, kama ambavyo yeye mwenyewe ameona; na hata Mheshimiwa Nderiananga, Naibu Waziri alikwenda kutembelea hospitali yetu ya mkoa hapa kuangalia mazingira hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, alijionea mwenyewe alichokisema Mheshimiwa Mbunge, kwamba sasa hivi kuna vitanda ambavyo Rais wetu ame-supply, unatumia remote, kinashuka kinamtolea mlemavu huduma kama ambavyo inatakiwa. Tutauzingatia huu ushauri wake aliousema hapa katika kwenda kununua hivyo vitanda na vifaa kama ambavyo ameshauri na tutaendelea kuchukua ushauri kutoka kwake. (Makofi)
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:- Je, hospitali ngapi zimetenga vyumba vya kujifungulia wanawake wenye ulemavu nchini?
Supplementary Question 2
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha vyoo vya watu wenye ulemavu vinawekwa kila wodi ya Mkoa wa Kagera, maana kuna vyoo vya kuchuchumaa tu? Ahsante.
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali zuri na hasa kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia shughuli za afya kwenye Mkoa wa Kagera. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamhakikishia tu kwamba kwanza, moja, kwa hizi shilingi bilioni 21 ni mojawapo ya fedha zinazoenda kuhakikisha zinaboresha maeneo hayo ambayo yana shida. Hospitali yake ya Mkoa imekuwa ikikusanya kila mwezi zaidi ya shilingi milioni 300 mpaka shilingi milioni 400. Hivyo, ninamwelekeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali, kwa kutumia mapato ya ndani aendelee kushughulikia maeneo yenye changamoto. (Makofi)
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:- Je, hospitali ngapi zimetenga vyumba vya kujifungulia wanawake wenye ulemavu nchini?
Supplementary Question 3
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kumekuwa na unyanyapaa mkubwa sana wa watoa huduma wanaotoa huduma eneo la kujifungulia ama shughuli nyingine za hospitalini kwa watu wenye ulemavu. Je, Serikali ina mkakati gani, kama ilivyo kwenye elimu, wa kuhakikisha kwamba wale watoa huduma wanapata mafunzo rasmi kwa ajili ya kuwahudumia watu wenye ulemavu?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge. Eneo hili ni nyeti sana na ndiyo maana unaona nimezungumzia hospitali za Taifa, kanda na wilaya. Ni maeneo ambayo tuna uhakika kwa 100% tayari mafunzo uliyoyasema yametolewa na miundombinu imewekwa pia. Sasa tunaelekea kwenye maeneo ya vituo vya afya na zahanati ili kuhakikisha si tu tunaboresha infrastructure lakini pia kubadilisha attitude ya watu na attitude ya wahusika wenyewe.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli unapozungumzia walemavu kuna walemavu wasioona wanahitaji namna ya kuwasaidia, wasiosikia namna ya kuwasaidia. Kuna mama mwingine anakuja ana ulemavu lakini pelvic girdle yake imekaa kiasi kwamba unajua huyu ni moja kwa moja kwenye operation na chuma cha operation ni kile kila ambacho unatakiwa u-operate wote. Hutakiwi kuwa-separate, kila mama um-treat kama mama, lakini kila mmoja ana specific need. Hata wale ambao si walemavu wanapokuja kwenye eneo la tiba ambao kabisa hawana ulemavu wowote lakini wote wanahitaji specific need kulingana na yeye mwenyewe, kwa sababu kila mtu ana mambo yake yaliyojificha ambayo ni siri ya madaktari. Kwa hiyo, kikubwa ni attitude lakini kum-attend kila mtu individually kulingana na mahitaji yake.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved