Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Geoffrey Idelphonce Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Primary Question

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo kipya na cha kisasa cha Polisi na kuboresha Makazi ya Askari Polisi Wilayani Masasi?

Supplementary Question 1

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana. Napenda kuishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri, hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kutokana na umuhimu wa kituo hiki cha polisi cha Masasi, ambacho kinahudumia Wilaya za jirani pamoja na Nchi jirani ya Msumbiji, especially pale kwenye mpaka. Wizara ipo tayari sasa kutoa mgao maalum wa angalau magari mawili ili kuongeza nguvu ya hilo jengo ambalo litajengwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, hivi karibuni tulipata dhahama kubwa sana pale Masasi Mjini kwa soko kubwa la Masasi kuungua moto. Je, Wizara hii ya Mambo ya Ndani ipo tayari kutoa mgao wa gari ya zimamoto ya kisasa kabisa ili kuweza kuongeza nguvu kwa wananchi wetu kuokoa mali zao? Ahsante.

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kutenga magari kwa ajili ya Wilaya ni nia ya Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, hususani Jeshi la Polisi, kuhakikisha Wilaya zake zote zinapata vitendeakazi yakiwemo magari, pikipiki na vifaa vingine. Kwa hivyo nimhakikishie tu kwamba sasa hivi tukamilishe ujenzi wa hicho kituo, lakini hatua itakayofuata ni kuwawezesha kwa vitendeakazi yakiwemo magari.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu soko lililoungua ni dhamira ya Serikali, hususani Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Zimamoto na Uokozi kupeleka vifaa vya kisasa katika Wilaya zake zote na Mikoa ambayo haikuwa nayo. Nadhani limejibiwa mara kadhaa hapa kwamba, Serikali imeingia makubaliano na nchi wahisani kwa ajili ya kupata fedha zitakazowezesha ununuzi wa vifaa vya kuzimia moto kwa ajili ya mikoa yote na wilaya zake zote. Nashukuru. (Makofi)