Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza ustawi wa familia kwa kuweka wanandoa waajiriwa katika vituo vya kazi vya jirani?

Supplementary Question 1

MHE. NG’WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa takwimu zinaonesha kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la ndoa nyingi zinazovunjika baada tu ya miaka miwili ya kufungwa kwake. Kufuatia takwa la Sheria za Ndoa la mwaka 1971, Serikali haioni haja ya kuondoa au kupunguza takwa hili au kigezo hiki cha miaka mitatu kwa waajiriwa wanaotafuta uhamisho kwa kigezo cha kufuata wenza wao? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa ni ukweli usiopingika kwamba malezi mazuri ya watoto na kuwepo kwa familia imara na bora kunategemea malezi ya wazazi wote wawili na sasa hivi nchini tumekuwa na changamoto kubwa sana ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto. Hatuoni haja au Serikali haioni haja ya kuondoa kabisa kigezo hiki cha miaka mitatu kwa watu wanaotafuta uhamisho? Au kuwaweka moja kwa moja waajiriwa ambao ni wanandoa sehemu moja ya ajira? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Kamani kwa namna ambavyo anafuatilia masuala ya haki za watumishi ikiwemo uhamisho.

Mheshimiwa Spika, katika kujibu swali lake anasema kwamba kigezo cha miaka mitatu kuondolewa, Serikali iliweka kigezo hiki cha miaka mitatu kwanza ili kuweka stability ya taasisi, kwa maana ya kwamba ukiruhusu watumishi wakakaa kwa muda mfupi namna ya ku-retain na performance ya taasisi inaweza kushuka. Hii imeoneshwa katika Mikoa ya Pembezoni baada ya kuweka muda mfupi watumishi wengi wanachukua check number na kuondoka na baadaye kupelekea uhaba wa watumishi.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Serikali imeendelea kutoa vibali vya uhamisho kwa wale watumishi hasa wanaotaka kuungana na wenzao. Kwa mwaka wa fedha 2023/2024, maombi yalikuwa takribani 3,374 na Serikali imetoa vibali 1,136. Kwa hiyo, Serikali itaendelea na jitihada hiyo bila kuathiri haki na maombi ya hawa watumishi wanaoomba kufuata wenza wao. (Makofi)

Name

Munira Mustafa Khatib

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza ustawi wa familia kwa kuweka wanandoa waajiriwa katika vituo vya kazi vya jirani?

Supplementary Question 2

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika, je, Serikali haioni haja ya kuongeza kigezo cha ‘mwenza wako’ wakati wa kuomba ajira ili kuwarahisishia watumishi kuwapangia mkoa ambao alikuwa anatoka mwenza wake na kuweza kupunguza gharama za kuhamisha watumishi hawa? Ahsante. (Makofi)

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, Serikali imetambua jambo hilo na ndiyo maana katika mwaka huu ajira zilizotangazwa 47,404, Serikali imewapa uhuru waombaji wa ajira hizo kuomba mikoa hiyo wanayotaka na lengo kubwa ni wao kwenda sehemu wanazotaka ili kuzuia wimbi hili la kuomba uhamisho kila wakati. Nakushukuru.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza ustawi wa familia kwa kuweka wanandoa waajiriwa katika vituo vya kazi vya jirani?

Supplementary Question 3

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niulize swali. Kwenye halmashauri nyingi ambazo sisi tunakutananazo Kamati ya LAAC kumekuwa na watumishi wanaokaimu muda mrefu kiasi kwamba wanashindwa kufanya maamuzi sahihi kutokana na kukaimu. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha mnajaza nafasi kwenye halmashauri zote nchini ili kuwe na ufanisi na utendaji kazi ambao unaridhisha? (Makofi)

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, suala la kukaimu ni kweli limelalamikiwa na Serikali tumelichukua kwa uzito mkubwa. Hivi sasa kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tuna zoezi la kufanya assessment nchi nzima kuona wale watumishi wanaokaimu katika nafasi mbalimbali. Wale watakaokuwa wamekidhi vigezo, tayari Serikali imeandaa utaratibu wa kuwa-confirm na wale ambao watakua hawajakidhi vigezo basi utaratibu mwingine wa kujaza nafasi zile utafanyika. Nakushukuru sana. (Makofi)