Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Primary Question

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA (K.n.y. MHE. RHODA E. KUNCHELA) aliuliza:- Kumekuwa na sintofahamu katika eneo la Kata ya Misunkumilo, Wilaya ya Mpanda Mjini, Wanajeshi wanadai eneo hilo ni la Jeshi, lakini makazi ya wananchi yalitangulia na wana hati ya maeneo yao:- Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kutatua jambo hili ikiwa Jeshi limewakuta wananchi katika eneo hili?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. La kwanza, katika mgodi wa JPM ambao uko katika Kata ya Mpanda Hoteli ilikuwa ni sehemu ambayo imewekwa mizinga ile ya kijeshi; lakini hapo hapo katika mgodi huo wa JPM kwa sababu wengi ni wawekezaji wageni, lakini wananchi wa mahali pale wanapata shida sana. Naomba Serikali iweze kutoa tamko kwa sababu wananchi hao wananyanyaswa.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, mimi natoka Mbeya, lakini pale Mbeya sehemu ya Mbalizi kuna Jeshi la Wananchi ambao wako pale na liko jirani sana na wananchi hususan Kata ya Iwindi na Utengule, Usongwe. Sasa nina wasiwasi kwamba lisije likatokea jambo ambalo lilitokea Mbagala. Serikali inatoa tamko gani kwa wananchi hawa ambao wanaweza wakapata madhara kama ya Mbagala? Ahsante.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI (K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mary Mwanjelwa anazungumzia unyanyasaji aliouita unyanyasaji ambao unafanywa na Jeshi la Wananchi kwenye mgodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, niombe hili jambo tulifanyie utafiti na tulichunguze uhalisia wake. Baada ya hapo ndiyo tutakapoweza kutoa tamko la Serikali. Sehemu ya pili, swali lake la pili kuhusiana na Mbeya ni kweli, baada ya kutokea matatizo yale ambayo yalitokea Mbagala, Serikali ilichukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kwamba inadhibiti matatizo kama yale yasijitokeze. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nichukue nafasi hii kuwahakikishia tu Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwa ujumla kwamba hatutarajii matatizo kama haya yajitokeze kwa sababu Serikali imechukua hatua madhubuti. Hata hivyo, hatutalidharau jambo hili ambalo amelizungumza Mheshimiwa Mbunge nalo pia tutalichukua, tulifuatilie kwa kina tuone kama kuna kasoro tuweze kuzifanyia kazi na kuzirekebisha.