Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aluliza: - Je, nini chanzo cha ongezeko la wagonjwa wa figo nchini?

Supplementary Question 1

MHE. JACQUELINE K. ANDREA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali.

Swali langu la kwanza, ni nini mpango wa Serikali kudhibiti matumizi holela ya dawa za binadamu ambayo imeonekana ni moja ya sababu inayochangia ugonjwa huu wa figo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, ni nini mpango wa Serikali kuwezesha hospitali zake kutoa huduma ya kusafisha figo ili kuondoa adha wanayopata wagonjwa wa figo katika huduma na gharama za matibabu? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge Kainja kwa namna ambavyo anafuatilia masuala ya afya, hasa kwenye Mkoa wa Tabora ambao wakati wote amekuwa akifuatilia hata masuala ya watu binafsi kuhakikisha mambo yanakaa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza, ni nini Serikali inafanya kuondoa matumizi holela ya dawa? Moja ni kuendelea kuelimishana na kutumia fursa hii kwamba matumizi ya dawa yazingatie maelezo ya daktari na unapokwenda kwenye duka la dawa, basi uwe umepata prescription ya daktari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi Waheshimiwa Wabunge mliona kampeni yetu na tumeleta katuni hapa inayozungumzia holela holela itakuletea matatizo. Maana yake tunaendelea na hilo suala la kuelimisha kuhusu alichosema dada yangu Mheshimiwa Kainja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, tunafanyaje kuhusu kuhakikisha tunawapunguzia wananchi mzigo wa matibabu hasa wanapopata matatizo wanapokwenda hospitali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, suala la Bima ya Afya kwa Wote na mmeona wiki hii Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwa Arusha akiwa kwenye tamasha kubwa sana la kujipanga kuhakikisha tunafikia suala la Bima ya Afya kwa Watu Wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunapambana kuhakikisha sasa vifaatiba, dawa na kila kitu tunakwenda kununua kiwandani moja kwa moja, badala ya kununua kwa wauzaji wa kawaida ili kushusha gharama ya matibabu kwenye maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali ina utaratibu na ndiyo maana kila hospitali ina Maafisa Ustawi wa Jamii ambapo wale watu wanaoshindwa kulipa, basi kuna utaratibu wa kufuata ili waweze kutibiwa bila malipo, ahsante. (Makofi)

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aluliza: - Je, nini chanzo cha ongezeko la wagonjwa wa figo nchini?

Supplementary Question 2

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama za kusafisha figo kwenye Hospitali Binafsi na Hospitali za Serikali ina utofauti mkubwa wa bei. Hospitali Binafsi zina unafuu ukilinganisha na Hospitali za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri ni kwamba ukienda kusafisha figo kwenye Hospitali za Serikali ni ghali zaidi kuliko Hospitali Binafsi; ni nini kauli ya Serikali kupunguza zaidi gharama hizi ili waathirika wa jambo hili waweze kupata unafuu na kupata matibabu? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa sababu kwa kweli kwenye eneo hili amekuwa akifuatilia karibu sana, lakini amekuwa akifuatilia sana wananchi wa kule Arusha kwa ukaribu sana hususani Karatu na amekuwa akinilitea wagonjwa wa namna hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba inategemea unazungumzia Hospitali Binafsi kwa level gani? Maana yake ukiwa na Hospitali Binafsi ambayo let say ni Polyclinic na unazungumzia Muhimbili, bado bei haisababishi kuwa kubwa na vile vifaa na tiba yenyewe, maana yake kuna mambo mengi yanayozingatiwa kulingana na level ya hospitali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamuomba Mheshimiwa Mbunge, nikimaliza kujibu swali tukae mimi na wewe unioneshe maeneo specifically ili nijue, tuangalie tatizo tulitatue kwa pamoja kwa sababu kwa kweli Hospitali za Serikali ndiyo inatakiwa iwe bei rahisi kuliko za private. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninataka kujua specifically ni nini, ili tuweze kushughulikia kwa pamoja. (Makofi)

Name

Kunti Yusuph Majala

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aluliza: - Je, nini chanzo cha ongezeko la wagonjwa wa figo nchini?

Supplementary Question 3

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri amesema kitu pekee ambacho kitaweza kutusaidia Watanzania kukabiliana na gharama kubwa za matibabu ni Bima ya Afya kwa Wote, lakini mpaka sasa mchakato bado unasuasua, Serikali haioni sasa ni wakati umefika wa kuwasaidia wagonjwa wetu hapa nchini kupunguza gharama ya usafishaji wa figo kutoka shilingi 300,000 mpaka shilingi 50,000? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakupongeza Mheshimiwa Kunti kwa swali hili zuri, lakini ninakuhakikishia dada yangu, wiki hii ulimuona Mheshimiwa Waziri Mkuu akiwa Arusha na aki-launch programu kubwa sana ambayo sasa inaenda kuanza ya kuhakikisha Watanzania wote wanaenda kuingia kwenye Bima ya Afya kwa Wote ambayo ndiyo suluhu kubwa kwa kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba Mheshimiwa Kunti, jinsi ambavyo anajipanga sasa hivi kurudi Bungeni, hivyo hivyo ninakuomba ujipange kuhakikisha wale wanaotakiwa kukurudisha Bungeni, wakati unawaambia nirudisheni Bungeni, basi nguvu hiyo hiyo utumie kuwashauri wakate kadi ya Bima ya Afya. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia siyo tu suala la Bima ya Afya, ninazungumzia ku-access vifaa kutoka viwandani moja kwa moja, itashusha gharama za matibabu. (Makofi)

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aluliza: - Je, nini chanzo cha ongezeko la wagonjwa wa figo nchini?

Supplementary Question 4

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, swali langu kidogo lilikuwa linafanana na la Mheshimiwa Paresso.

MWENYEKITI: Kwa hiyo limeshaulizwa?

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka niliboreshe kidogo; gharama za kusafisha figo pale Muhimbili ambayo ni Hospitali ya Serikali ni shilingi 180,000 kwa section moja, lakini ili mgonjwa wa figo akae vizuri, anatakiwa kusafisha figo mara tatu kwa wiki, hii ni shilingi 540,000 kwa wiki. Kwa Mtanzania wa kawaida ni pesa nyingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hoja yangu ilikuwa, ni lini Serikali itapunguza gharama za kusafisha figo kwenye Hospitali za Serikali? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mbunge kwa kweli kwenye eneo hili ninajua anazungumzia, kwa sababu physically anajua anavyoniletea wagonjwa wenye matatizo yao, namna ya kusaidiana pamoja. Kwa kweli anafuatilia sana masuala yanayohusu watu kwenye eneo la afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamwambia tu tumeanza, ndiyo maana ukienda baadhi ya hospitali sasa katika hospitali zetu za mikoa, hospitali mbili sasa za Mkoa wa Dar es Salaam tumefanikiwa kuhakikisha tunashusha na ndiyo maana Mheshimiwa Waziri wa Afya sasa ameunda timu, inapitia kuja na itemization zote ili tujue tunapunguza wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu unaweza ukapunguza, badala ya kupunguza ukaua mfumo wenyewe na kuua mfumo wenyewe unaweza ukasababisha watu wakose huduma kabisa. Ni bora wapate huduma kwa ghali, lakini waendelee kuwa hai wakati tunaangalia mambo yanakwendaje. Kwa kweli tunalichukua hilo, tunaenda kulifanyia kazi na timu imeanza kufanya kazi, wiki ijayo wanaleta ripoti watupe way forward ya kupunguza gharama.

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aluliza: - Je, nini chanzo cha ongezeko la wagonjwa wa figo nchini?

Supplementary Question 5

MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kuniona. Asilimia tatu mpaka saba ya watu wanasumbuliwa na tatizo la figo na miongoni mwa watu hawa ni watu maskini kabisa wasiokuwa na uwezo. Asia Mohamed anaishi bila figo kwa miaka 17 na wazazi wake wote hivi sasa wamefariki, ni yatima yuko kitandani anasubiri kifo.

Je, uko tayari Mheshimiwa Waziri, kusaidia binti huyu mdogo aweze kupata huduma ya kusafishwa figo ambayo ameshindwa kumudu tuweze kuokoa maisha yake? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge, lakini nina mambo machache ya kumwomba; moja, kwanza ni kweli huyo dada amekaa miaka 17 akiwa na hilo tatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, maana yake inaonesha ni kwa namna gani mifumo yetu ya afya ni mizuri kiasi kwamba mtu anaweza asiwe na figo, lakini bado akaishi bila kuwa na figo. Kwa maana ya kwamba anatibiwa vizuri kwenye hospitali zetu, wengine saa nyingine figo zina-reject mara nyingi, anarudiwa mara nyingi, lakini anaendelea kuwa salama na kuishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa issue ni tunamsaidiaje? Kaka yangu Mheshimiwa Shigongo, pili ninakuomba suala siyo tutatibuje figo, suala ni kwamba tunakingaje watu wasipate matatizo ya figo, kwa sababu wewe ni mtu ambaye uko katika tasnia ya habari, ninakuomba pia utusaidie kutumia vyombo vyako vya habari ili kuhakikisha tunahamasisha elimu ya watu kuishi maisha ambayo hayatawasababisha wapate matatizo kama hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Mheshimiwa Mbunge amlete huyo tutamfanyia exemption, ninaanza kwa kusema hapa miezi minne kwanza tutaanza naye atatibiwa bure wakati tunatafuta solutions zingine. (Makofi)

Name

Halima James Mdee

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aluliza: - Je, nini chanzo cha ongezeko la wagonjwa wa figo nchini?

Supplementary Question 6

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri amesema mwenyewe vizuri kabisa kwamba kinga ni bora kuliko tiba. Vijana wengi sasa hivi wanapata ugonjwa wa figo kwa sababu kuna pombe kali zenye sumu zimesambaa na zinauzwa kwa bei ndogo sana. Sasa kwa sababu umesema kinga ni bora, ni lini Serikali mnaanza operation mahsusi ili kuweza kuondoa pombe zote za aina hii Tanzania, ili tuweze kuokoa kizazi cha sasa na kijacho? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze tu Mheshimiwa Halima Mdee, wakati wote amekuwa ni mtu mwenye uwezo wa kutafakari vitu kwa kina sana na kutazama kwa mapana. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niseme tu kwamba ni kweli pombe zinasababisha matatizo mengi siyo masuala ya figo tu na hata wakati mwingine ukienda mezani ukisoma utaona mahali pameandikwa tumia pombe kwa akili, wengine anaandika matumizi ya pombe ni mabaya chini ya miaka 18 usitumie, hizo zote ni juhudi ambazo zinafanywa, lakini ni katika hali halisi ni masuala ya kubadilisha tabia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninawaomba kama ambavyo nimesema Wabunge wengi hapa sisi tuna influence sana, tutumie influence zetu kuhamasisha watu kwamba wanahitaji kuishi maisha salama hata kama kuna vitu vyenye madhara, lakini bado vinatumika, basi kila mtu awe makini kwenye kutumia. Ninachukua suala lako kwa sababu linahusu sekta mbalimbali, tuendelee kwa pamoja kushirikiana, tutaenda kushirikiana na sekta mbalimbali tuje na way forward ya pamoja ya kutoa hamasa kubwa kukinga hayo mambo. (Makofi)