Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 1

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ilishatoa maeneo na Mheshimiwa Mbunge wa eneo husika alikidhi vigezo ambavyo Wizara ilileta kwa ajili ya kutoa maeneo ni kwa nini mpaka sasa maghala hayo hayajengwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili halmashauri nyingi nchini zimekuwa zikinufaika na cess ya mazao yanayotolewa kwenye halmashauri zote zinazonufaika na mazao hayo. Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wakulima ili kuwajengea maghala wakishirikiana na halmashauri ambazo wananufaika na cess? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kama nilivyojibu katika swali langu la msingi ni kwamba katika mwaka wa fedha unaokuja ndipo tunaanza ujenzi wa maghala katika maeneo yote ambayo tumeainisha. Kwa hiyo, jambo hili anavyosema lini? Ni kuanzia mwaka wa fedha unaokuja.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kujenga maghala ndiyo jukumu kubwa ambalo tunalifanya sisi kama Wizara kwa kushirikiana na halmashauri pamoja na wakulima kupitia AMCOS zao ili tuhakikishe kwamba wananufaika na hii faida ambayo wanaipata kwa wao kushiriki katika kilimo, ahsante sana. (Makofi)

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 2

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana nini mkakati wa Serikali kupitia Ushirika kukarabati maghala yaliyokuwa yakitumika kuhifadhi pamba na pembejeo yaliyochakaa sana Jimboni Busanda? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, moja ya mkakati tulionao ni pamoja na maghala ambayo yako katika eneo la Jimbo la Busanda katika mwaka wa fedha unaokuja tutayakarabati, ahsante. (Makofi)

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 3

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, teknolojia ya kuhifadhi hii nafaka katika mifumo ya tabaka tatu ndiyo teknolojia ambayo inaweza ikamudu katika ngazi ya kaya lakini ni ghali. Serikali ina mpango gani kupunguza bei ya mifuko hiyo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachokizungumza Mheshimiwa Mbunge na moja ya mkakati tulionao sisi kama Wizara ni kuhakikisha kwamba tunafuta fedha ili tuweke ruzuku katika hiyo mifuko ili tuwapunguzie adha wakulima, ahsante. (Makofi)

Name

Simon Songe Lusengekile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busega

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 4

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Spika, pale kwenye Kata ya Mwamanyili na Kata ya Ngasamo kuna maghala ya ushirika ambayo yamechakaa je, Serikali iko tayari kuja kufanya ukarabati kwenye maghala haya ili yatumike kuhifadhia chakula? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante, katika mwaka wa fedha unaokuja, sehemu ya maghala tutakayojenga ni pamoja na maeneo ya Busega. Kwa sababu lengo la Serikali ni kuongeza uhifadhi wa chakula kutoka tani laki tano kufikia tani laki saba mwakani kwenda tani milioni 1.2 katika mwaka wa fedha unaofuatia, ahsante. (Makofi)

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 5

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ina wakulima wengi; Mheshimiwa Waziri tayari tuna eneo la kujenga maghala kwa ajili ya kuwasaidia Wakulima wa Mbogwe; je, lini Serikali mtatoa pesa ili kusudi mkawajengee Wakulima wa Mbogwe maghala? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge, kwanza nimepokea ombi lake lakini la pili nitangalia katika mpango kama upo katika mwaka wa fedha huu unaofuatia na kama halipo tutahakikisha kwamba linawekwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 ili tuhakikishe Wananchi wa Mbogwe nao wanajengewa ghala, ahsante. (Makofi)

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 6

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru ni lini mtalipa cess ambayo Halmashauri ya Mji wa Makambako tunawadai shilingi milioni 250 ili ikidhi matarajio ambayo bajeti yake…
SPIKA: Mheshimiwa, weka kisemeo vizuri ili uingie kwenye Taarifa Rasmi za Bunge. Uliza tena swali lako.

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, ni lini Serikali italipa shilingi milioni 250 kwenye Halmashauri ya Makambako ambayo ni cess ya makusanyo ya ambayo walikuwa wananua mazao ya mahindi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ni kwamba kuna halmashauri zinazotudai cess ikiwemo Makambako hata Wanging’ombe pamoja na halmashauri nyingine na madeni yao yote tumeshapeleka Wizara ya Fedha tunasubiri tu fedha ambayo itatoka Wizara ya Fedha na sisi tutahakikisha tunawalipa kwa wakati, ahsante. (Makofi)

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 7

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, ni lini Mkoa wa Simiyu utajengewa maghala ya kutosha ya kuhifadhia mazao?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante, katika mpango tulionao katika mwaka wa fedha unaokuja kuna halmashauri kadhaa ambazo tunajenga katika Mkoa wa Simiyu. Kwa hiyo niseme tu katika mwaka unaokuja watapata maghala mapya, ahsante. (Makofi)

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 8

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, ahsante, Serikali kupitia Bodi ya Korosho ilianza kujenga maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru tangu 2014 na ujenzi ule ulikwama kwa muda mrefu na mpaka sasa bado haujaweza kuendelea, ni lini ujenzi huu utaendelea ili kupata maghala ya kuhifadhia mazao? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante, katika mpango wa mwaka wa fedha unaokuja 2024/2025 maghala yalioko katika Jimbo na Halmashauri ya Tunduru yapo katika mpango wetu. Kwa hiyo mwakani tutakwenda kuyamalizia, ahsante.

Name

Salma Rashid Kikwete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mchinga

Primary Question

MHE. MOSHI S. KAKOSO K.n.y. MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao katika Halmashauri ya Ushetu?

Supplementary Question 9

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa Jimbo la Mchinga ni miongoni mwa Majimbo yanayozalisha ufuta kwa wingi na kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amesema atajenga maghala; je, Jimbo la Mchinga litakuwa ni miongoni mwa maghala hayo yatakayojengwa? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimwondoe shaka mama yangu, Mama Salma Kikwete, Wananchi wa Mchinga ninaamini tutawafikia. Nitakwenda kuangalia katika mpango kama haipo sasa hivi tutahakikisha tunaweka katika mwaka wa fedha unaokuja, ahsante sana. (Makofi)