Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwantum Dau Haji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza kasi ya ujenzi wa Vituo vya Polisi nchini?
Supplementary Question 1
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, ahanste sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri aliyoyatoa hapo lakini nina maswali yangu mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa baadhi ya maeneo nchini havijafikiwa kujengwa vituo vya polisi, lini Serikali itajenga vituo hivyo? (Makofi)
Swali langu la pili, sambamba na ujenzi wa vituo vya polisi, vipi kuhusu ujenzi wa nyumba za askari nchini? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa vituo vya polisi ambavyo havijafikiwa nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwenye mwaka wa fedha 2024/2025 tunajenga vituo vya polisi 12 na tunamalizia maboma 77 ambayo tayari yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini. Pia, kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani tunajenga vituo 26 kutoka kwenye bajeti pamoja na Mfuko wa Tuzo na Tozo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, Serikali imeendelea kujenga nyumba za askari katika maeneo mbalimbali na itaendelea kutenga fedha na kujenga nyumba awamu kwa awamu na kukamilisha katika maeneo ambayo hayana nyumba za askari. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza kasi ya ujenzi wa Vituo vya Polisi nchini?
Supplementary Question 2
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wananchi wa Tarafa ya Njinjo wamekuwa wakisafiri umbali wa zaidi ya kilomita 100 kufuata huduma za Kipolisi Kilwa Masoko.
Je, ni lini Serikali itawajengea Kituo cha Polisi?
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Francis Ndulane kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi, tayari tunajenga vituo vya polisi awamu kwa awamu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama kwenye mwaka wa fedha huu kituo chake hakipo basi kwa mwaka wa fedha unaokuja tutatenga fedha na kujenga kituo cha polisi katika eneo ambalo amelitaja Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza kasi ya ujenzi wa Vituo vya Polisi nchini?
Supplementary Question 3
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, Kata ya Susuni ni moja kati ya Kata ambazo zipo pembezoni kabisa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, nataka kujua ni lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi ukizingatia Kata jirani ya Mwema ina vituo viwili vya polisi?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama niliyosema tunajenga vituo vya polisi vya Kata kwa awamu. Kwa mwaka wa fedha huu 2024/2025 tunajenga vituo 12, lakini hii ni kwa awamu ya kwanza, kwa mwaka unaofuata tutajenga vituo 196 na vinakuja vituo 212.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kituo chako kama hakipo kwenye mpango wa mwaka huu tutapanga mwaka wa fedha unaokuja ili kujenga kituo cha Polisi cha Kata ya Susuni kama ambavyo umeomba. (Makofi)
Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza kasi ya ujenzi wa Vituo vya Polisi nchini?
Supplementary Question 4
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, Halamshauri ya Itigi, Kituo cha Polisi Itigi, Polisi wa Itigi wanakaa kwenye majengo ya Reli na Reli wanajiimarisha pia yamechakaa sana.
Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kujenga kituo cha polisi katika Halmashauri ya Itigi? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Massare kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema tunajenga vituo vya polisi kwa kutumia bajeti ya Serikali, Mfuko wa Tuzo na Tozo lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama kituo chake mwaka wa fedha huu hakipo basi tutakitengea fedha kwenye mwaka wa fedha 2025/2026 ili tujenge kituo cha polisi katika eneo lake la Itigi, ahsante sana.
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza kasi ya ujenzi wa Vituo vya Polisi nchini?
Supplementary Question 5
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuwa wananchi wa Kiteto, Kata ya Magungu, Kijungu na Lengatei wameshaonesha nia ya kujenga vituo vya polisi. Lini Naibu Waziri utakuwa tayari kutembelea vituo hivi?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nipo tayari kwenda Kiteto kutembelea vituo hivyo ambavyo vimeshaanza kujengwa na wananchi, kama nilivyosema maboma yote ambayo wananchi wameshaanzisha, Serikali ipo tayari kumalizia kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Tumetenga shilingi bilioni 3.8 kwa ajili ya kazi hiyo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nitakuja kukutembelea katika eneo lako. (Makofi)