Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Justin Lazaro Nyamoga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itaangalia upya mipaka ya Tarafa ya Makambako ambapo kata 12 zipo Jimbo la Makambako na kata tano zipo Jimbo la Lupembe?
Supplementary Question 1
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, Mji wa Makambako unakuwa na idadi ya watu inaongezeka na kutokana na hivyo maeneo yamekuwa madogo kwa hiyo upimaji wa viwanja na maeneo kwa ajili ya makazi na shughuli nyingine yanakosenaka.
Je, ni lini Serikali itafanya mpango wa kuongeza lile eneo ili wananchi wa Makambako waendelee kupata makazi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuna maeneo mengi sana kwenye nchi hii ambayo ugawaji wake haukuzingatia jiografia na kwa hiyo huwa ni shida sana kwenye utoaji wa huduma, kwa mfano mtu wa kutoka Tarafa ya Mazombe na Mahenge Ilula, maeneo ya Ilula kwenda Kilolo kupata huduma inabidi apite Iringa Mjini. (Makofi)
Je, Serikali ina mpango gani wakupitia maeneo haya na kuona jinsi nzuri ya kuyafanya yawe katika uwiano wa kijiografia ili kurahisisha huduma za wananchi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kuna baadhi ya halmashauri au majimbo ambayo yana changamoto ya kimipaka, lakini kwa Jimbo la Makambako Mheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga amefuatilia mara kadhaa kuongeza mipaka ya Jimbo la Makambako, Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niitumie nafasi hii kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, lakini pia Mheshimiwa DC kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kufuata utaratibu wa kupata maoni kwa wananchi wa maeneo hayo ili waweze kupeleka kwenye vikao vyao vya DCC na vikao vya RCC na kukubaliana kama wilaya, lakini kama mkoa na kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa ajili ya kuchukua hatua na hili linakwenda sambamba na ile hoja ya baadhi ya mipaka kutozingatia hali za kijiografia za maeneo hayo na kuleta changamoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itapokea maoni kutoka kwa wadau na wadau hao ni wananchi wa maeneo hayo kwa maana ya DCC pamoja na RCC kwa ajili ya kuchukua hatua hizo, ahsante. (Makofi)
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itaangalia upya mipaka ya Tarafa ya Makambako ambapo kata 12 zipo Jimbo la Makambako na kata tano zipo Jimbo la Lupembe?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali fupi la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto iliyopo Makambako, inafanana sana na changamoto ambayo tunayo kule Arumeru Mashariki, hususani mpaka wa Jimbo letu la majimbo mawili ya upande wa Mashariki kwa maana ya Siha na Hai. Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu changamoto hiyo ya mpaka? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirejee kwamba ni Serikali inashauri mamlaka husika kwa maana ya DCC na RCC kukaa na kutoa mapendekezo, lakini mipaka ya Majimbo inatolewa pia na ya Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa hiyo, naomba wafuate taratibu hizo kuleta maoni yao ambayo yamefuta sheria na kanuni za mwongozo ulivyo ili tuweze kuona namna gani mamlaka husika zitachukua hatua kurekebisha changamoto hizo ikiwa inawezekana kufanya hivyo, ahsante.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itaangalia upya mipaka ya Tarafa ya Makambako ambapo kata 12 zipo Jimbo la Makambako na kata tano zipo Jimbo la Lupembe?
Supplementary Question 3
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa kama vile ikituchanga hivi. Unasema tupeleke mipaka ya Halmashauri Bunda na Halmashauri ya tunapokaa Jimbo la Bunda lipo tofauti. Tukapeleka vikao vyote kwenye kikao cha DCC na tukapeleka RCC na tumeleta mapendekezo yetu hapa, lakini majibu yanayotoka ni kwamba Serikali sasa hivi haina mpango wa kuendeleza mipaka ya utawala, huku tunaambiwa tupeleke.
Sasa nini jibu la Serikali kuhusu mipaka hii ili tusiwe tunapiga kelele humu ndani? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwanza ilishatoa maelezo na msimamo kwamba kipaumbele kwa sasa ni kuboresha maeneo ya utawala yaliyopo ili yaweze kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. Hii ni kwa sababu tuna kata, tuna halmashauri, tuna Ofisi za Wakuu wa Wilaya, kuna Ofisi za Wakuu wa Mikoa na makazi yao bado hayakamilishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya hoja ambayo Waheshimiwa Wabunge, mara kwa mara wanaitoa hapa ni kwamba maeneo hayo yanahitaji kujengewa miundombinu ili maeneo hayo ya utawala watoe huduma bora zaidi.
Kwa hiyo, Serikali iliona ni vyema kuweka kipaumbele cha kukamilisha miundombinu hiyo kwenye mamlaka ambazo tayari zinafanya kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea haijasimama, kwa maana ya taratibu nyingine za kuomba kubadili mipaka, kuomba mamlaka mpya zinaendelea na document hizo zinatunzwa, muda ukifika tutazipitia document hizo na kufanya maamuzi kulingana na vigezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Getere kwamba yote ni sawa kwamba, tuendelee na kule maombi hayo kwa kufuata taratibu na Serikali itaendelea kuyatekeleza kulingana na vipaumbele, lakini pia muda ukifika hatua nyingine zitachukuliwa katika maeneo hayo mengine, ahsante.
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itaangalia upya mipaka ya Tarafa ya Makambako ambapo kata 12 zipo Jimbo la Makambako na kata tano zipo Jimbo la Lupembe?
Supplementary Question 4
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, Wilaya ya Kishapu ina kata 29, lakini ina idadi ya watu 355,000 na ukubwa wa eneo ni kilometa za mraba 45,333; eneo hili ni kubwa sana na kimsingi Serikali ni lazima irahisishe kupeleka huduma kwa wananchi kwa kupunguza eneo la kitawala na hasa kijimbo.
Je, Serikali inasema nini ili kupunguza eneo hili na kuwa na majimbo mawili walau kuwarahisishia wananchi huduma za kimaendeleo? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie nafasi hii kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Butondo kwamba Serikali inatambua kwamba, Halmashauri ya Kishapu na Jimbo la Kishapu, ni miongoni wa majimbo makubwa na ameshawasilisha hoja hiyo mara kadhaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nirejee kumhakikishia tu kwamba, Serikali itachukua hatua hizo baada ya kupata taarifa rasmi kupitia vikao vya DCC na RCC na kuwasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI na pale ambapo utaona sasa kuna sababu ya kufanya hivyo na muda mwafaka basi hatua hizo zitachukuliwa. Kwa hiyo, nikuhakikishie kwamba Serikali inatambua na tutachukua hatua hizo kadri itakavyowezekana, ahsante. (Makofi)