Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y. MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:- Je, ni lini vijiji vyote vya Mkoa wa Singida vitaunganishiwa umeme?

Supplementary Question 1

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina swali moja la nyongeza. Sisi kule kwetu Mtwara, kwenye majimbo ya Tandahimba, Newala Vijijini pamoja na Lulindi bado kuna vijiji vingi havijapatiwa umeme. Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha vijiji vile ambavyo vimebaki vinapatiwa umeme kwa haraka? Nakushukuru. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba, vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme na kama ambavyo mmeidhinisha bajeti ya Wizara husika, yapo mafungu yametengwa, kwa ajili ya kazi hiyo. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge wawe na subira, jambo hili litakamilika kama tulivyoahidi.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y. MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:- Je, ni lini vijiji vyote vya Mkoa wa Singida vitaunganishiwa umeme?

Supplementary Question 2

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Je, ni lini Serikali itaanza mradi wa usambazaji wa umeme kilometa mbili katika Jimbo la Babati Vijijini?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari mikakati ipo katika hatua za mwisho kuhakikisha kwamba, umeme unafikishwa katika Jimbo la Babati Vijijini. Namuomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira wakati tunatekeleza jambo hili. (Makofi)

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y. MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:- Je, ni lini vijiji vyote vya Mkoa wa Singida vitaunganishiwa umeme?

Supplementary Question 3

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona. Wilaya ya Ngara, vijiji 14 bado havijawasha umeme. Ningependa kujua ni lini Serikali itawasha vijiji hivyo, ili kuwaondolea adha wananchi? (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kule Ngara vijiji 14 havijawashiwa umeme. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali tunayo mikakati ya kuhakikisha kwamba, ndani ya kipindi kifupi vijiji vyote nchini, siyo hivyo vya Ngara tu, lakini vijiji vyote nchini vitapatiwa umeme. (Makofi)

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y. MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:- Je, ni lini vijiji vyote vya Mkoa wa Singida vitaunganishiwa umeme?

Supplementary Question 4

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona. Ninafahamu kwamba, sasa tayari tumeshawasha mtambo namba mbili wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa hiyo, tatizo la umeme limeisha. Ni nini kinasababisha kukatika-katika kwa umeme katika baadhi ya maeneo kwa sasa? (Makofi)

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, Serikali imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme unaimarika kutokana na kuongezeka na kuzalishwa kwa umeme kupitia Bwawa la Mwalimu Nyerere. Vilevile, kama ambavyo tumekuwa tukisema mara nyingi hapa, miundombinu yetu ya kusambaza umeme na yenyewe imekuwa na changamoto kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hii ndiyo ambayo inachangia katika kukatika-katika kwa umeme, lakini kama ambavyo tumeonesha kwenye bajeti yetu, Serikali imetenga fedha nyingi, kwa ajili ya kuboresha usambazaji wa umeme kwa kuboresha njia za usambazaji. Namuomba Mheshimiwa Mbunge na wananchi wawe na subira wakati tunakamilisha utengenezaji wa miundombinu hii. (Makofi)