Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itarejesha utoaji wa ruzuku ya pembejeo za dawa kwa wakulima wa kahawa?
Supplementary Question 1
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali kwa majibu mazuri. Pamoja na majibu hayo, miche wanayoigawa huwa ina ukinzani wa magonjwa na siyo wadudu. Sasa kwa kuwa wakulima wengi hawawezi kumudu kununua viuatilifu vya wadudu, je, Serikali ina mpango gani wa kuhamasisha matumizi ya dawa za kiasili kama vile utupa, ili kukabiliana na wadudu wanaoharibu kahawa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kahawa huwa inahitaji maji mengi sana na maji haya yamekuwa yanapatikana kupitia mifereji ya asili. Je, Serikali ina mikakati gani ya kuwasaidia wananchi wa Jimbo langu la Moshi Vijijini kurekebisha mifereji ya asili, ili waweze kumwagilia kahawa zao ukiwepo ule Mfereji wa Makeresho ambao ulikuwepo kwenye bajeti? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, cha kwanza, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge, Profesa Ndakidemi, kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo lake la Moshi Vijijini, hususan katika kuhamasisha kilimo cha kahawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi namthibitishia kwamba, nimezungumza na wataalamu na tumekubaliana kwamba, sisi tutakuwa tayari kuhamasisha hususan matumizi ya dawa za asili, ili kutoondoa ubora wa kahawa ambayo inazalishwa kwa wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara tuko tayari kusajili watu wote ambao wanazalisha viuatilifu vya asili, kama ambavyo wanafanya bio-plants walioko Moshi na tumekubaliana tutanunua kwa ruzuku katika mwaka unaokuja karibu lita 20,000. Kwa hiyo, hiyo ndiyo mipango na mikakati ya Serikali, ili kuhakikisha tunawasaidia watu wa zao la kahawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mifereji. Tulishaliweka katika bajeti yetu na sasa hivi tunachokifanya ni kuendelea tu kupitia, ili tuje tutafute mkandarasi tuweze kuiboresha na kuwa ya kisasa, ili wananchi waweze kumwagilia kipindi chote na wapate maji ya uhakika, ahsante sana. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itarejesha utoaji wa ruzuku ya pembejeo za dawa kwa wakulima wa kahawa?
Supplementary Question 2
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Wananchi wa Tarafa ya Nambis katika Jimbo la Mbulu Mjini wanajitahidi sana kulima zao la kahawa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapelekea miche bora ya kahawa kupitia ruzuku ya Serikali, ili waweze kuleta tija zaidi? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Namuambia tu kwamba, miche tunayo, muda wowote wakulima waje tuwakabidhi. Ndiyo maana unaona hata kwenye jibu la msingi, tumezalisha miche milioni 21.89 na tumegawa yote bure. Kwa hiyo, watufikie tu na sisi tutaifikisha. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved