Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:- Je, kati ya mwaka 2021 – 2022 Serikali ilianzisha miradi mingapi mipya ya umwagiliaji ili kukuza kilimo cha mpunga katika Jimbo la Kilombero?

Supplementary Question 1

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na nashukuru majibu ya Serikali na huyo Mkandarasi ambaye Mheshimiwa Waziri alinikabidhi alisema pia atafanya study ya namna gani ya kupunguza mafuriko katika Mto Lumemo, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza, Serikali imetujengea mradi wa umwagiliaji Mkula, Kata ya Mkula na Godauni la Kata ya Mkula zaidi ya miaka miwili sasa godauni hilo halijakamilika kwa sababu Mkandarasi hajalipwa pesa zake. Je, ni lini Serikali itamlipa Mkandarasi huyu ili akabidhi godauni kwa wananchini? (Makofi)

Swali la pili, juzi nikiwa ziara Jimboni nimezungumza na wakulima wa miwa, mpunga, wabeba mizigo, wenye mashine za kukoboa, makuli wanaomba sana kuzungumza na Mheshimiwa Waziri Bashe, wanampenda sana. Je, ni lini Mheshimiwa Waziri Bashe atafanya ziara Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Mji wa Ifakara? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kwamba, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kilombero kwamba mkandarasi ambaye anatengeneza ile Scheme ya Mkula pamoja na godauni lake ni kwamba tumepata zile document zake kwa ajili ya malipo na zimeishatufikia, kwa hiyo kinachofanyika sasa hivi tu ni mchakato, tumeishazipeleka Wizara ya Fedha wapo katika hatua za mwisho, wakishamaliza maana yake atalipwa ili aweze kumalizia ule mradi na kukabidhi kwa wananchi. Kwa hiyo, jambo hili Mheshimiwa Mbunge tunalifahamu na tunalo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Waziri kufika amesikia, akishindwa kufika yeye mimi mwenyewe nitafika, ahsante. (Makofi)