Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, kampuni gani zilishiriki ununuzi wa kahawa Mkoani Kagera kwa mwaka 2023?

Supplementary Question 1

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, ninataka kujua mkakati wa Serikali wa kuzisaidia AMCOS, badala ya kuuza kahawa ghafi (dry cherry) wakauza fine coffee ambayo inaitwa FAQ. Sababu ni kwamba FAQ bei ya dry cherry ni ndogo ukilinganisha na FAQ. Kama hii inauzwa shilingi 5,000 kama mnada ulivyo leo, FAQ inauzwa shilingi 10,000 kwenye masoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuuza FAQ wataweza kupata faida ya mbolea ambayo wanakuwa wanainunua baada ya kuuza hizo kahawa ambayo ni maganda. Ninataka kujua mkakati wa Serikali wa kuzisaidia hizo AMCOS ili ziweze kuuza FAQ kwa faida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kampuni ambazo zimekuwa zikinunua specialized coffee wakati mwingine huenda moja kwa moja kwenye AMCOS na hununua bei ndogo ukilinganisha na bei ya minada. Ni nini kauli ya Serikali kuzitaka zile kampuni kununua bei sawa na mnada tofauti na ilivyo leo au zaidi ya hapo? Ninakushukuru. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, jambo la kwanza tu nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi Serikali moja ya mikakati yetu ni kuhakikisha kwamba tunazi-empower hizi AMCOS. moja kwa ku-invite wawekezaji wengi kuja kutengeneza viwanda hapa nchini ambapo watakuwa na nafasi ya kuongeza thamani ya kahawa na kuuza kwa bei nafuu. Kwa hiyo, hilo jambo tunalo na tunalifanyia kazi na tumeunda Tume maalumu kwa ajili ya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bei ndogo inayonunuliwa katika hizo AMCOS katika maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja kwenye hivi vyama, kauli ya Serikali ni kwamba sasa hivi tumetangaza matumizi ya mnada wa TMX na tumewataka Vyama vya AMCOS vitumie ule mnada ili kupata bei ambayo inaridhisha. Haturuhusu sana watu kwenda kununua moja kwa moja kwa mkulima kwa sababu wamekuwa wakiwanyonya.

Kwa hiyo, huo ndio msimamo wa Serikali na tutaendelea kusimamia. Kwa hiyo, kikubwa hapa kwa taarifa uliyotoa, sisi tutaendelea kufuatilia ili jambo hili lisiendelee, ahsante. (Makofi)

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, kampuni gani zilishiriki ununuzi wa kahawa Mkoani Kagera kwa mwaka 2023?

Supplementary Question 2

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kufahamu ni nini mkakati wa Serikali kuweka utaratibu wa kuuza vanila, hususani mkoani Kagera? Ahsante.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, mkakati wa Serikali wa sasa ni kwamba zao la vanila tumeliingiza kati mnada wa TMX kwa maana linauzwa kwa mnada na kwa mfano tulikuwa kule Kyela pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu, tulienda kuzindua msimu wa ununuzi wa vanila kupitia mfumo wa TMX. Kwa hiyo, mfumo ule siyo tu utatumika Kyela ni kwamba utatumika katika maeneo yote wanayozalisha mazao ya vanila ikiwemo Kagera, ahsante. (Makofi)

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, kampuni gani zilishiriki ununuzi wa kahawa Mkoani Kagera kwa mwaka 2023?

Supplementary Question 3

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, katika Kata ya Ukwega yaani Vijiji vya Mkalanga, Makungu, Lulindi na Ukwega yenyewe kuna kilimo cha kahawa, lakini wanakatishwa tamaa na ukosefu wa soko, kwa hiyo zao lile linaelekea kuondoka katika eneo lile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ipo tayari kupeleka wataalamu na kuangalia njia bora ya kwanza kukiimarisha kilimo kile, lakini pili kupata soko ili waendelee na kilimo cha kahawa? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Nyamoga kwamba Serikali tupo tayari, moja tutaleta wataalamu na hili lipo ndani ya uwezo wetu, lakini pili tutaendelea kutafuta masoko, lakini soko kubwa sasa hivi tunatumia mnada, lakini vilevile tunazungumza na balozi zetu kuleta wawekezaji zaidi kwa ajili ya kutengeneza viwanda ndani vya kuongeza thamani ya zao ambayo ndiyo yatakuwa moja ya sehemu ya masoko makuu ya kahawa ambayo inazalishwa nchini, kwa hiyo, hilo lipo na tunaliweza, ahsante.

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, kampuni gani zilishiriki ununuzi wa kahawa Mkoani Kagera kwa mwaka 2023?

Supplementary Question 4

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali kama Serikali ina mikakati gani mahususi ya kutafuta wanunuzi na masoko yenye tija kwa wakulima wa kahawa Tanzania?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimjibu tu Mheshimiwa Profesa Ndakidemi, Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini kwamba moja ya mkakati wetu mkubwa, kwanza ilikuwa ni kumuondoa mkulima wa kahawa katika ule utaratibu wa uuzaji wa kahawa wa zamani, ambapo sasa hivi zao la kahawa linauzwa kwa kupitia njia ya TMX kwa maana mnada ambapo wanunuzi wanakutana pamoja na ku-bid price na yule ambaye ana-tender kwa bei ya juu ndiyo anayepewa nafasi ya kununua zile kahawa, kwa hiyo, huu ni mkakati wa kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wetu wa pili sasa hivi tumeshazungumza na balozi zote nchini ambazo wamekuwa na jitihada kubwa ya kutafuta masoko ya kahawa yetu kule nje ya nchi ambako ndiyo wamekuwa watumiaji wakubwa, hii naamini kwamba itasaidia kuongeza bei ya zao la kahawa na tumekuwa tukifanya hivyo na mabalozi wamekuwa wakitupa mrejesho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaamini kuna promising future kwenye zao la kahawa, kwa hiyo tuwatake wakulima wote waendelee kuzalisha kahawa kwa wingi na sisi kama Serikali kupitia taasisi zetu za TARI tutaendelea kutoa mbegu bure za kahawa ili kulifanya zao hili liendelee kuleta fedha nyingi sana za kigeni hapa nchini, ahsante. (Makofi)

Name

Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, kampuni gani zilishiriki ununuzi wa kahawa Mkoani Kagera kwa mwaka 2023?

Supplementary Question 5

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, watu wasishangae kumwona Mbunge wa Kinondoni anaulizia swali la kahawa, hatulimi kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa mujibu wa Jarida la Coffee Review, Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa kahawa Afrika na ni nchi ya 14 duniani, tuna sifa nzuri, lakini ukienda kwenye maduka ya unywaji kahawa huko Europe na sehemu nyingine huikuti kahawa ya Tanzania ikitangazwa kama ilivyo kahawa ya Colombia, Brazil, Kenya na Uganda. Ni nini kauli ya Serikali katika kuifanya kahawa yetu ya Tanzania itangazwe na isifike duniani? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze vilevile Mbunge wa Kinondoni kwa kuuliza swali hili la kimataifa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kikubwa tu nimthibitishie Wizara ya Kilimo tukishirikiana na watu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia taasisi zao hususani TanTrade wamekuwa wakienda katika yale masoko makubwa kutangaza bidhaa hizi, lakini vilevile kupitia balozi zetu na miongoni mwa zawadi kubwa ambazo tumekuwa tukizitoa kwa marafiki zetu zile nchi ambazo tumekuwa tukitembelea ni pamoja na kupeleka bidhaa za kilimo hususani kahawa na korosho katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ile yote tu ni sehemu ya moja ya kutangaza, kwa hiyo tu niseme kwamba tutaongeza mkazo na msisitizo pamoja na bajeti ili kuhakikisha sasa kahawa ya Tanzania iwe inanyweka katika maeneo mengi hapa nchini, ahsante.

Name

Philipo Augustino Mulugo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songwe

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, kampuni gani zilishiriki ununuzi wa kahawa Mkoani Kagera kwa mwaka 2023?

Supplementary Question 6

MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na mimi niweze kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imetokea hivi karibuni kule Songwe baadhi ya kampuni zinakuja kununua ufuta kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa Mfumo wa TMX, lakini wametokea matapeli baadhi ya kampuni wanataja bei kubwa na AMCOS na wakulima wanakubali wanauza ufuta kwa kutumia njia ya minada safi. Baada ya siku mbili au tatu kadiri ya sheria hawalipi fedha na wanapotea na wakulima wanabaki wanahangaika. Nini kauli ya Serikali ya kudhibiti makampuni haya kwa nini wasiwa-blacklist au kuwafungia kabisa? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, anachokizungumza Mheshimiwa Mulugo ni jambo ambalo sisi kama Wizara ameshatufikishia na kama Wizara tupo katika hatua za kulifanyia kazi, lakini kitu cha kwanza ambacho nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge, sasa hivi kama Wizara tutafanya due diligence kwenye kwa maana uhakiki kabla ya zile kampuni kwenda kununua, ama ku-bid kwa wakulima kwa sababu mtu anapo-bid bei ya juu na akishindwa kuwalipa wakulima maana yake anawarudisha nyuma wakulima katika maeneo husika.

Kwa hiyo, jambo hili lipo na tutalitolea taarifa yake kamili kwa sababu lipo katika mchakato wa kuhakikisha kwamba tunadhibiti hizi changamoto ambazo zimejitokeza, ahsante. (Makofi)

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: - Je, kampuni gani zilishiriki ununuzi wa kahawa Mkoani Kagera kwa mwaka 2023?

Supplementary Question 7

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Kwanza kabisa naipongeza Serikali na hasa nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuzindua huo mpango wa kununua vanila kwa njia ya mnada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa palikuwa hakuna soko la uhakika kwa ajili ya ununuzi wa vanila, mkoani Kagera wakulima wamelizwa mwaka jana kuna mtu amejitokeza amechukua vanila zote, lakini hakumlipa mkulima hata mmoja. Je, Serikali mna mpango gani kuwasaidia hao wakulima wa vanila Mkoa wa Kagera waweze kulipwa hizo hela ambazo walidhulumiwa tangu mwaka jana? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ni kwamba moja ya hatua ambayo tutachukua ni kwamba huyo mnunuzi ambaye alinunua vanila na hakuwalipa wananchi maana yake sisi kama Wizara tutamwita na ikibidi tutachukua hatua za kisheria, lakini jukumu letu kama Serikali ni kuhakikisha fedha yoyote ya mkulima inalipwa na hilo sisi tutalifanya. Kwa hiyo nimwondoe tu shaka Mheshimiwa Mbunge na wakulima wa Kagera kwamba jambo hilo limetufikia na tunalifanyia kazi, ahsante.