Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Primary Question

MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Mabanda – Handeni?

Supplementary Question 1

MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia maswali ambayo nimekuwa nikiyauliza hapa Bungeni siku zilizopita, Serikali ilielekeza kuanza kwa mchakato wa kuipandisha hadhi Zahanati ya Hedi - Kwamagome ili kuwa kituo cha afya.

Je, mchakato huo utakamilika lini ili sasa zahanati hii ya Hedi kiwe kituo kikubwa cha afya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, ni kweli Mheshimiwa Reuben Kwagilwa amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na maombi ya Halmashauri ya Mji wa Handeni kupandisha hadhi ya Zahanati ya Kwa Hedi - Kwamagome kuwa kituo cha afya. Naomba nimhakikishie kwamba tayari tumeshatuma wataalamu na taarifa imeshaletwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, zahanati ile inakidhi vigezo vya kupanda hadhi kuwa kituo cha afya, kilichobaki sasa tunaandaa utaratibu wa kupata fedha kwa ajili kwenda kuanza ujenzi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kituo hicho cha afya kitapandishwa hadhi. (Makofi)

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Mabanda – Handeni?

Supplementary Question 2

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, Kata ya Muhinda katika Jimbo la Buhigwe ni miongoni mwa kata ambazo zina sifa na vigezo vya kujengewa kituo cha kata.

Je, Kata ya Muhinda ni miongoni mwa kata mojawapo ambazo zitajengewa kituo cha afya kama ulivyozungumza?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, Kata ya Muhinda katika Jimbo la Buhigwe ambalo linawakilishwa na Mheshimiwa Kavejuru, ni moja ya kata ambazo Mheshimiwa Mbunge amefuatilia mara kadhaa na tayari Serikali imeshaweka kwenye orodha ya kata za kimkakati ambazo zitapelekewa fedha ndani ya mwaka huu wa fedha katika mpango wa kituo cha afya kila jimbo, kata hiyo imeingizwa. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kavejuru kwamba tayari fedha inaandaliwa na tutahakikisha kwamba tunapeleka fedha hiyo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya, ahsante. (Makofi)

Name

Ghati Zephania Chomete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Mabanda – Handeni?

Supplementary Question 3

MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia jengo la zahanati lililojengwa katika Kata ya Mkoma, Wilaya ya Rorya kwa nguvu za wananchi mpaka kufikia hatua ya kupaua?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, zahanati ambayo imejengwa katika Kata ya Mkoma katika Jimbo la Rorya, ni kweli, kwanza nichue nafasi hii nimpongeze sana Mheshimiwa Ghati Zephania Chomete kwa namna ambavyo amefuatilia kuhusiana na jambo hili, pia niwapongeze sana wananchi wa kijiji hiki kwa kutoa nguvu zao na nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua jitihada za wananchi na itaingiza kwenye mpango wa kuweka fedha mapato ya ndani au Serikali Kuu kwa ajili ya kuunga mkono nguvu za wananchi na kukamilisha zahanati hiyo, ahsante. (Makofi)

Name

Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Primary Question

MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Mabanda – Handeni?

Supplementary Question 4

MHE. TWAHA A. MPEMBWENE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Kibiti tuna kituo cha afya cha muda mrefu na tunaishukuru sana Serikali kwa maboresho yanayoendelea kufanyika katika eneo hilo, je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa maabara katika kituo hiki cha afya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, Kituo cha Afya cha Kibiti ni kituo cha afya kikongwe na kinahudumia wananchi wengi katika Kata ya Kibiti na maeneo ya jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Mheshimiwa Twaha Mpembwene amefuatilia mara kadhaa. Naomba nimhakikishie Mbunge na wananchi wa Jimbo la Kibiti kwamba Serikali hii sikivu ya Dkt. Samia Suluhu Hassan itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara hizo pia na ukarabati wa majengo hayo ambayo tayari ni chakavu, ahsante. (Makofi)