Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Jeshi la Polisi nchini linafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda usalama wa raia na mali zao, lakini linakabiliwa na upungufu mkubwa wa makazi kwa Askari wake:- (a) Je, Serikali imepanga kujenga majengo mangapi katika Wilaya Mpya ya Itimila na Busega kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017? (b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuyakamilisha makazi ya Askari Polisi yaliyomo Wilaya ya Meatu?
Supplementary Question 1
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na majibu ya Naibu Waziri. Wilaya ya Busega, Itilima na Kituo cha Polisi cha Mwandoya kilichopo Jimbo la Kisesa katika Wilaya ya Meatu, Askari wa Jeshi la Polisi wanaishi katika mazingira magumu. Nikisema mazingira magumu namaanisha hata zile nyumba za wananchi ni za shida sana kupatikana kwa ajili ya kupanga. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri katika mikoa aliyopanga kutembelea yuko tayari kutembelea Mkoa wa Simiyu ili aweze kujionea namna Askari wa Jeshi la Polisi wanavyoishi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; Wilaya ya Meatu ilianzishwa mwaka 1986 na majengo hayo yalijengwa mwaka 1999, yapata sasa ni miaka 17. Majengo hayo yameanza kuchakaa na kuoza, lakini kwa mujibu wa majibu ya Naibu Waziri, nimeona hata kwenye ule mgawo wa nyumba 4,136 majengo hayo hayamo. Je, Serikali sasa haioni haja ya kukamilisha majengo hayo na kuweza kuyanusuru?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, kwamba niko tayari kutembelea Wilaya ya Busega? Jibu, niko tayari. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kwamba, katika mradi wa nyumba 4,136, Wilaya ya Busega na Itilima haimo. Ukweli ni kwamba, katika Mkoa Mpya wa Simiyu katika mradi wa nyumba 4,136 tunatarajia kujenga nyumba 150. Sasa nadhani sasa hivi kwa concern ambayo ameonesha Mheshimiwa Mbunge, tujaribu kuangalia sasa katika mgawo wa nyumba 150, tuhakikishe kwamba, zinakwenda katika Wilaya ya Busega na Itilima ili kukabiliana na changamoto kubwa ya makazi ambayo Mheshimiwa Mbunge amelizungumza na sisi tunalifahamu.
Name
Doto Mashaka Biteko
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukombe
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Jeshi la Polisi nchini linafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda usalama wa raia na mali zao, lakini linakabiliwa na upungufu mkubwa wa makazi kwa Askari wake:- (a) Je, Serikali imepanga kujenga majengo mangapi katika Wilaya Mpya ya Itimila na Busega kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017? (b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuyakamilisha makazi ya Askari Polisi yaliyomo Wilaya ya Meatu?
Supplementary Question 2
MHE. DOTO M. BITEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Kwa kuwa, matatizo yaliyoko Itilima yako vilevile Bukombe na Kituo cha Polisi cha Uyovu ambacho kinahudumia Wilaya za Bukombe, Biharamulo na Chato kiko kwenye hatari ya kuanguka wakati wowote kwa sababu jengo lile limechakaa. Je, Waziri anatuambia nini wananchi wa Bukombe juu ya Kituo hicho ambacho kina hali mbaya sana?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua kwamba, tuna changamoto kubwa sana ya vituo nchi nzima. Tuna vituo vibovu vingi tu na tuna sehemu nyingi ambazo hata vituo hamna. Takribani tunahitaji ujenzi wa vituo vipya kama 4,119 hivi kwa hesabu za haraka haraka, kwa hiyo tuna changamoto kubwa na tunafahamu kwamba kwa kutekeleza ujenzi wa vituo vyote na kukarabati vituo vyote nchi nzima kwa wakati mmoja si jambo jepesi, tutakuwa tukifanya hivyo hatua kwa hatua.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana nimezungumza katika maswali mbalimbali niliyokuwa nikijibu, kwamba tuna mpango wa kuweza kurekebisha vituo hivyo awamu kwa awamu. Kwa hiyo, niseme tu Mheshimiwa Mbunge ni kwamba kwa kuwa amesimama hapa na ame-raise hii hoja ya kituo chake, basi tutajitahidi kadri ambapo uwezo utaruhusu ili tuweze kukikarabati kituo hiki.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved