Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bernadeta Kasabago Mushashu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo la kuwatenga walioathirika na magonjwa ya mlipuko Kagera?
Supplementary Question 1
MHE. BENARDETA K. MASHASHU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninaishukuru Serikali kwa kutujengea hicho kituo kidogo pale Mutukula cha kuwatenga wanaohisiwa kwamba wana magonjwa ya mlipuko kule Mtukula, Wilayani Missenyi.
Je, ni lini sasa Serikali itaona umuhimu na kujenga vituo vya namna hivyo kwenye mipaka pale Mulongo – Kyerwa, Rusumo pamoja na Kabanga kule Ngara?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Mkoa wa Kagera umepakana na nchi jirani kadhaa, kwa hiyo, ni rahisi kupata haya magonjwa ya mlipuko kama Marburg na Ebola, je, ni lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kutujengea hospitali kubwa ya magonjwa ya kuambukiza (infectious disease hospital) kusudi hao wanaotambulika kwenye hivyo vituo (isolation centers) kama ya Mutukula wapate mahali ambapo wataenda kupata matibabu? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge sio tu kwa sababu ya swali lake hili, lakini kwa sababu ya kazi ambayo tumekuwa tukifanya pamoja kwa miaka yote hii minne kwa ajili ya Wana-Kagera, lakini kwa ajili ya wanawake wa Mkoa wa Kagera.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni lini tutaweza kujenga maeneo kama hayo kwenye maeneo mengine. Kwa kweli fedha zinaendelea kutafutwa sio tu kwenye maeneo ya Mkoa wa Kagera, lakini ni mipakani kote Kigoma, upande wa Kusini na kila mahali kuhakikisha tupo vizuri inapofika kuna magonjwa ya mlipuko kwa majirani zetu ili tuweze kujikinga pia.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kujenga hospitali kubwa, moja, kwanza Mkoa wa Kagera una hospitali moja kubwa ya Mkoa na Hospitali hiyo kubwa inaendelea kupanuliwa na kuwa kubwa zaidi na kuwekewa mambo mbalimbali kwa sababu kikubwa sio kujenga hospitali ya magonjwa ya kuambukiza, kikubwa ni kuhakikisha hayo magonjwa hayaingii Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka kuwahakikishia jinsi uhitaji unapoonekana tutaenda kufanya hayo, lakini nataka kukuhakikishia hospitali yenu ya mkoa itaenda kupanuliwa na kuwa kubwa sana na kuwa na vitengo vya magonjwa mbalimbali yanayosibu watu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved