Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:- Je, lini TBS itaweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na biashara ya kusindika vyakula?

Supplementary Question 1

MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza nini mpango wa TBS kuhakikisha inawasaidia wajasiriamali wadogo kupata alama ya bidhaa zao, alama za ubora za bidhaa zao kwa gharama nafuu lakini pia kwa muda mfupi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili, TBS ina mkakati gani kuhakikisha inafungua vituo vya kutoa huduma kwa wajasiriamali wadogo hususan kwenye maeneo ambayo hayawezi kufikika kwa urahisi. (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi ni dhamira ya Serikali ya TBS kuwaimarisha hawa wajasiriamali wadogo na ndiyo maana utaona tumeweza kuwafikia zaidi ya 14,354. Sasa kwa sababu kama ilivyoelezwa huenda kutokana na ukubwa wa eneo analotoka la Dar es Salaam wajasiriamali ni wengi tutaimarisha TBS kwa sababu makao makuu yake yapo Dar es Salaam kuwafikia kwenye ngazi za Wilaya ili wengi zaidi waweze kupata huduma kwa gharama nafuu, ninashukuru.

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:- Je, lini TBS itaweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na biashara ya kusindika vyakula?

Supplementary Question 2

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Kwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa kama vile chakula vinywaji na madawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu siyo waaminifu kwa kuendelea kuuza bidhaa ambazo zimeisha muda wake. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi hasa kule chini kuzuia kuendelea kutumia bidhaa hizo na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi wetu? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Amar kwamba wapo wafanyabiashara wasiyo waaminifu ambao huweza kuuza bidhaa zilizopitwa na muda wake kwa kulijua hilo na kwa sababu Mamlaka ya Udhibiti wa Viwango ipo makao Makuu Dar es Salaam kwa mujibu wa Sheria ya Viwango, mamlaka za wilaya kwa maana ya halmashauri wataalamu wake wamekasimiwa majukumu ya ukaguzi wa bidhaa katika maduka, pharmacies na kadhalika ili kuwabaini watu hao na kuchukua hatua stahiki. Kweli wanapobainika hatua kali huchukuliwa ikiwa ni pamoja na uharibifu wa bidhaa hizo na kuwafikisha Mahakamani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kupitia hadhira hii nihimize Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambao wamekasimiwa jukumu hili…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kwa kifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: …wamekasimiwa jukumu hili kulitekeleza kwa umakini ili kuondoa malalamiko kama haya, ninashukuru.

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:- Je, lini TBS itaweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na biashara ya kusindika vyakula?

Supplementary Question 3

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa elimu ya usindikaji wa chumvi na magadi ambayo yanapatikana kwa wingi Ziwa Gendabi na Balangdalalu ili wananchi wa maeneo hayo waweze kunufaika na rasilimali zinazopatikana kwenye maeneo yao?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninatambua umuhimu wa Serikali kuwasaidia wasindikaji wadogo wakiwemo wa chumvi na magadi kwa kutambua umuhimu huo ndiyo maana Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanda Vidogo (SIDO) hutoa mafunzo ya mara kwa mara kwenye maeneo yetu mbalimbali ikiwemo Hanang ili wafanyabiashara wa namna hii waweze kupata utaalamu wa kusindika chumvi kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Serikali,ahsante!