Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi?
Supplementary Question 1
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Kata ya Mlowo ina wakazi zaidi ya laki sita na wakazi hao wote wanahudumiwa na zahanati moja tu na sisi kama Wabunge tumekuwa tukiomba sana kuweza kupatiwa Kituo cha Afya kwenye Kata ya Mlowo. Sasa nilitaka niiulize Serikali kwa nini sasa haijaona umuhimu wa kutenga hizo fedha kwenye mwaka wa fedha ujao? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Kalembo pamoja na Malangali kwenye Wilaya ya Ileje? Ahsante. (Makofi)
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Serikali imeweka mpango mkakati wa ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati ikiwemo Kata hii ya Mlowo – Mbozi. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba fedha ambayo itatengwa mwaka wa fedha 2025/2026 ni muda wa matazamio kwa maana ya maximum duration ambayo tumeweka, lakini tunaweza tukapata fedha wakati wowote na kupeleka kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo hiki cha afya. Kwa hiyo, nimtoe shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tunatambua umuhimu wa kituo hiki na tunaendelea kutafuta fedha ili twende kujenga kituo hiki.
Mheshimiwa Spika, lakini pili kuhusiana na Kituo cha Afya cha Malangali na katika kata hiyo nyingine naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tulishawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuanisha maeneo ya kata za kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kwa kata zile ambazo zinakidhi vigezo. Kwa maana ya idadi ya wananchi, umbali kutoka kituo cha afya cha karibu zaidi lakini pia na hali ya kijiografia. Kwa hiyo, kama Kata hizi zinakidhi vigezo hvyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, Ofisi ya Rais – TAMISEMI tutachukua orodha yake tuweke kwenye mpango mkakati kwa ajili ya kwenda kujenga vituo hivyo, ahsante. (Makofi)
Name
George Ranwell Mwenisongole
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbozi
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi?
Supplementary Question 2
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, naomba nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa nini kwenye hiki Kituo cha Afya cha Mlowo Serikali inakuwa na majibu mengi tofauti tofauti? La kwanza mlituambia kwamba mimi nilipouliza kama Mbunge wa Jimbo mlisema itajengwa kwa kutumia fedha za World Bank. Leo dada yangu Mheshimiwa Juliana Shonza ameuliza unatuambia kitajengwa 2026. Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokuja Mbozi alipiga simu TAMISEMI tukakubaliana kuna fedha zimekuja za ujenzi wa Serikali zitaenda kujenga kwenye hiki Kituo cha Afya cha Mlowo sasa kituo kimoja cha afya majibu matatu, sisi tushike lipi kwenye hili jibu?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mwenisongole, amefuatilia kwa karibu sana kuhusiana na Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Mlowo na nimewasiliana naye mara kadhaa na nimemhakikishia tu kwamba Serikali ina vyanzo vingi na vyanzo mbalimbali vya ujenzi wa vituo vya afya.
Mheshimiwa Spika, tuna vyanzo vya World Bank ambavyo tunatarajia wakati wowote fedha zikipatikana zitakwenda kwenye vituo vilivyoainishwa, lakini tuna mipango ya Serikali kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya miaka inayofuata 2024/2025 na 2025/2026 na hata tukipeleka fedha za World Bank mwaka huu wa fedha ujao bado tuna awamu ya pili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mlowo. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mbunge hii ni faida kwake kwamba tuna mpango wa World Bank fedha zikipatikana kituo hiki kitaanza kujengwa wakati wowote kama nilivyosema kwenye majibu yangu ya msingi.
Mheshimiwa Spika, lakini tuna mpango wa 2025/2026 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa kituo hicho ili kiweze kuwa fully na kuweza kutoa huduma vizuri zaidi. Kwa hiyo, majibu ya Serikali ni yale yale, dhamira ni ile ile kujenga Kituo cha Afya cha Mlowo na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutakwenda kujenga Kituo hicho, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved