Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anna Richard Lupembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nsimbo

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itamalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Itenka – Nsimbo?

Supplementary Question 1

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru kwa hili swali ambalo limejibiwa.

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Itenka sasa hivi kina takribani ya miaka miwili na kila siku tukiuliza kuhusu fedha zilizobaki kwa sababu tuliahidiwa milioni 850, lakini mpaka sasa hivi zimeletwa milioni 480, kiasi ilichobaki ni kingi. Wananchi wa Itenka wanatamani sana ile hospitali iweze kukamilika.

Je,ni lini Serikali itaweza kukamilisha? (Makofi)

Katika Kata ya Ugala kuna Kituo cha Afya, nacho tuliahidiwa milioni 850 mpaka sasa hivi zimekuja milioni 500. Je, ni lini Serikali wataleta fedha za Kituo cha Afya cha Ugala? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninampongeza Mheshimiwa Mbunge Mama Anna Richard Lupembe amefuatilia kwa karibu sana kuhusiana na fedha za awamu ya pili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Itenka na Ugala. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, wakati wa ujenzi huo wa vituo hivi vya afya tuliweka mpango wa kujenga vituo hivi kwa awamu.

Mheshimiwa Spika, awamu ya kwanza tulipeleka milioni 500 kwa vituo vyote kote nchini na imekamilika majengo yale matano ya awamu ya kwanza. Awamu ya pili tutakwenda pia kwa vituo vyote ambavyo vimekamilika awamu ya kwanza kwa ajili ya majengo mengine kama wodi za wanaume, watoto na wanawake kawaida. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, vituo hivi viwili ambavyo vimeshapata fedha za awamu ya kwanza, tutakamilisha kwanza majengo ambayo hayajakamilika ya awamu ya kwanza na baadae tutaingia kwenye awamu ya pili na nimhakikishie kwamba, tutapeleka fedha kwa ajili ya kazi hiyo, ahsante. (Makofi)

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itamalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Itenka – Nsimbo?

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Ikola ni miongoni mwa vituo ambavyo vimejengwa na Halmashauri ya Wilaya.

Je, ni lini watapelekewa fedha za kukamilisha hicho kituo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, niwapongeze Halmashauri ya Tanganyika kwa kujenga Kituo cha Afya cha Ikola kwa mapato ya ndani na niombe kumuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri kutuletea taarifa rasmi ya kiasi cha fedha ambacho wanahitaji ili Ofisi ya Rais, TAMISEMI itafute fedha na kupeleka kwa ajili ya ukamilishaji.

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itamalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Itenka – Nsimbo?

Supplementary Question 3

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Je, Serikali ina mapango gani wa kuipandisha hadhi zahanati ya Toangoma kuwa Kituo cha Afya kwa kuwa Kata ya Toangoma ina idadi kubwa ya watu. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Tulikwishatoa maelekezo na mwongozo unaelekeza hatua za kufuata kwa zahanati ambazo zina sifa ya kupandishwa hadhi kuwa vituo vya afya. Kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kumuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, kufanya tathmini kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Halmashauri na Mganga Mkuu wa Mkoa, kuona kama vigezo vyote kwa maana ya eneo na idadi ya wananchi vinakidhi kuwa na zahanati na kupandishwa hadhi kuwa kituo cha afya ili tuweze kuanza hatua za upandishaji wa kituo cha afya. (Makofi)

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itamalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Itenka – Nsimbo?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Je, ni lini Serikali itatenga fedha za kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nyarioba kama ilivyoahidi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali iliahidi na ni maelekezo ya Mheshimiwa Makamu wa Rais aliyatoa tukiwa kwenye ziara kule Kigoma, Nyarioba. Tayari tumeshakiweka kwenye orodha ya vituo ambayo vitapata fedha za umaliziaji kupitia Benki ya Dunia.