Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omar Ali Omar

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Wete

Primary Question

MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya mapitio katika kubaini kaya maskini ili kuondoa malalamiko?

Supplementary Question 1

MHE. OMAR ALI OMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwenye Jimbo langu la Wete kuna wananchi ambao wametolewa katika mfuko huu kimyakimya. Je, Serikali inafahamu mpango huo?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuongozana nami baada ya kumalizika kwa Bunge hili ili kwenda kuona na kutatua changamoto ambazo zimejitokeza katika jimbo langu kwenye Mfuko huu wa TASAF?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Omar Ali kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia masuala haya yanayohusu TASAF.

Mheshimiwa Spika, kuhusu wananchi wake kuondolewa kimyakimya, utaratibu uliopo ambao umewekwa na TASAF ni kwamba, wale wanaohitimu na kuimarika kiuchumi, kabla hawajaondolewa, kwanza wanapewa mafunzo na kuwaandaa na baadaye kupewa taarifa rasmi kwamba sasa mmefikia kwenye ukomo. Kama jambo hilo limetokea jimboni kwake, naomba kuchukua fursa hii kumwelekeza Mtendaji Mkuu wa TASAF afuatilie jambo hili na kama hawa hawakutaarifiwa, waweze kupata taarifa kufuatana na taratibu tulizoweka.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kufuatana naye kwenda jimboni, hili halina shaka, tukimaliza Shughuli za Bunge hapa tutaenda huko Pemba ili tukaone namna ya kuzungumza na kutatua changamoto hizi kwa pamoja. Ninakushukuru.

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya mapitio katika kubaini kaya maskini ili kuondoa malalamiko?

Supplementary Question 2

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa TASAF haiwezi kugusa maskini wote wa Tanzania na kwa kuwa maskini waliopo ni wengi sana sana wakiwemo vijana waliomaliza vyuo ambao hawana kazi bado wanategemea wazazi; wakiwemo wanawake ambao wanangoja kuguswa tu ili waweze kufanya miradi, wakiwemo pia hata akinababa ambao hawawezi kumudu chakula kwenye nyumba zao. Je, Serikali haioni sasa ni wakati wa kutoa miradi midogomidogo kwa makundi hayo niliyotaja badala ya kusema wote wakaguswe na TASAF? Ahsante. (Makofi)

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Kama Programu ya TASAF ilivyo, ina programu ambayo tulianza 2012 – 2019 na tuko awamu ya pili katika kunusuru kaya maskini ambayo itaenda 2019 mpaka 25 Septemba, mwakani. Serikali ina utaratibu mzuri, kuna namna ambavyo inawezesha haya makundi kwa mfano kupitia halmashauri kuna mikopo ya 4:4:2 na yote hii ni namna ambayo Serikali imejipanga namna ya kuwakwamua wananchi katika umaskini.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo na pamoja kwamba kuna Programu ya TASAF, bado pia Ofisi ya Waziri Mkuu ina programu ya mikopo kwa vijana ambayo inafanya ushirikiano pia pamoja na TASAF ambao wale vijana wanaotoka kaya maskini, wanaoshindwa, wanamaliza darasa la saba na kutokufanikiwa kwenda kidato cha kwanza, wameunganishwa na programu ya kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu kupata mikopo ya kusomeshwa VETA bure. Ninashukuru. (Makofi)

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya mapitio katika kubaini kaya maskini ili kuondoa malalamiko?

Supplementary Question 3

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, TASAF kwa kweli bado ni tatizo kubwa katika jimbo langu. Wengi waliomo mle hawastahili na walioachwa ndiyo wanastahili. Ninaomba kama akipata nafasi tuweze kuongozana naye kwenda Mwibara ili kuondoa hili tatizo ambalo limejitokeza, je, yuko tayari? Ninakushukuru.

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Kajege kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, utaratibu wa kuwapata wanufaika wa kaya maskini ulifanyika kupitia mikutano ya vijiji. Kwa hiyo vijiji na wananchi ndiyo waliamua nani anufaike na nani asiingie kwenye kunufaika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo TASAF kwa maana ya TASAF waliletewa watu ambao tayari wamepitia katika michakato ya kijiji. Kama kuna tatizo kwenye jimbo lako Mheshimiwa Kajege, kupitia Bunge hili ninaomba kumuahidi tutafika huko ili tuone namna ya kutatua changamoto hii.