Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Anania Tadayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwanga
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itafungua na kuanza kutumia Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, lililojengwa Ndea, Mwanga?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina swali moja tu la nyongeza. Tarehe 27 na 28 Disemba, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mwanga na Ofisi ya Mbunge wa Mwanga ikishirikiana na Kampuni ya Kisangara Tours tumeandaa tamasha la utalii, ambapo mojawapo ya maeneo yatakayopitiwa katika marathoni ni lango hili la Ndea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, lango liko tayari na barabara iko tayari kilichobaki ni kuimarisha tu ipitike misimu yote. Je, yuko tayari kuwahakikishia wananchi wa Mwanga kwamba, kabla ya tarehe 27 na 28 Disemba lango hilo litafunguliwa ili tamasha letu la marathoni liweze kufika kwenye lango la Ndea? Ahsante. (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, timu yetu inayoshirikiana na wilaya kufanya maandalizi, ikiwemo Ofisi ya Mbunge, inashughulikia jambo hili. Nimhakikishie kwamba, uzinduzi wa lango hili utakuwa sehemu ya shughuli hiyo ya tamasha kuanzia tarehe 27 na 28 Disemba.
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itafungua na kuanza kutumia Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, lililojengwa Ndea, Mwanga?
Supplementary Question 2
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha barabara zilizoko ndani ya hifadhi zetu, kwa mfano, Barabara ya kutoka Ngorongoro kuelekea Serengeti ambayo ni mbovu sana?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali inafanya kazi ya kuboresha kilometa 400 zilizoko ndani ya hifadhi zetu. Nimhakikishie kwamba, barabara aliyoitaja tunaipa kipaumbele kwa sababu, ni barabara muhimu sana kwa ukuaji wa utalii wa nchi yetu.
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itafungua na kuanza kutumia Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, lililojengwa Ndea, Mwanga?
Supplementary Question 3
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Wizara ya Maliasili, Waziri aliahidi kutuletea mizinga ya nyuki, Yaeda Chini, je, ni lini ahadi hii itatekelezwa?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la usambazaji wa mizinga ya nyuki linashughulikiwa na litakapokuwa tayari tutawataarifu. Ahsante.
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, lini Serikali itafungua na kuanza kutumia Lango la Kaskazini la Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, lililojengwa Ndea, Mwanga?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itafungua barabara na lango la Seleto kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa Kata za Leguruki na King’ori kiuchumi? Nakushukuru.
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu, ameuliza ni lini, naomba baada ya hapa tukutane na Mheshimiwa Mbunge, ili tuweze kulijadili jambo hili. Tuweze kumpa majibu ya uhakika.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved