Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Mbinga?
Supplementary Question 1
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naishukuru Serikali kwa majibu, lakini kama Serikali ilivyokiri kwamba jengo hilo lilijengwa mwaka 1969, ni wazi kwamba jengo hili limechakaa na lipo katika hali ambayo siyo nzuri sana ukilinganisha na majengo mengine yanayojengwa sasa hivi katika maeneo yetu ya wilaya. Bado nasisitiza Serikali ione umuhimu wa kujenga jengo jipya katika eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja la nyongeza, Kata za Mpepai, Mbangamao, Kikolo, Kihungu pamoja na Kagugu ziko mbali, nyingine zaidi ya kilometa 40 kutoka Mbinga Mjini. Kwa hiyo, bado kuna changamoto kubwa ya kupata huduma za kimahakama katika maeneo haya. Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inajenga jengo la Mahakama ya Mwanzo katika maeneo hayo niliyoyatamka?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakiri kwamba uwekezaji kwenye sekta ya Mahakama haukujitokeza kuwa na kipaumbele katika miaka mingi iliyopita, lakini kufuatia mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Sita ambapo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza zaidi masuala ya haki jinai kuwafikia wananchi, kipaumbele sasa ni kujenga Mahakama hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa ya Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge kwa ujumla, hivi sasa katika mwaka ujao, tunajenga Mahakama Jumuishi, Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki vinane kwa maana zile Mahakama ngazi ya mkoa zinazochukua, zinajumuisha kuanzia Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Hakimu Mkazi mpaka Mahakama Kuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, tunazo Mahakama za Wilaya mpya ambazo zinajengwa jumla 23. Pia tuna Mahakama za Mwanzo zitakazojengwa 78. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunda, nakiri kwamba kwenye eneo lako, kata zilizo mbali namna hii, Mahakama itaona uwezekano wa kuingiza kwenye mpango wake wa ujenzi ili eneo hilo liweze kupata Mahakama, ahsante.
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Mbinga?
Supplementary Question 2
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kuniruhusu kuuliza swali la nyongeza. Fedha za kujenga Mahakama ya Wilaya ya Uyui zipo, naogopa sasa bajeti inaisha, bado mwezi mmoja. Lini Serikali itaanza kujenga Jengo la Wilaya ya Uyui?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakiri kwamba ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, fedha zipo na hatua iliyofikiwa sasa hivi ni ya kumpata mkandarasi. Napenda kumhakikikishia, kwa sababu Mahakama imeona changamoto hiyo, hivi sasa Mtendaji Mkuu wa Mahakama kupitia idara zake za manunuzi, wanaharakisha michakato ya manunuzi ili Mahakama hiyo ujenzi wake uweze kuanza mara moja pamoja na Mahakama nyingine.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved