Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza Kampeni ya kunawa mikono ili kudhibiti magonjwa ambukizi?

Supplementary Question 1

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa uzinduzi wa hii kampeni ni juzi tu mwezi huu, lakini kabla ya hapo mlipuko wa COVID-19 ulikuwa umeleta aina fulani ya hali ya juu ya usafi katika nchi yetu. Maji yalikuwepo kila mahali ya kunawia mikono katika misikiti, kanisani, shuleni na hata hapa Bungeni. Jambo hilo limeisha tu baada ya kutangazwa COVID imekwisha. Swali la kwanza; je, Serikali ina mpango gani wa kusimamia na kuona kwamba, usafi ule unarejeshwa mara moja? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa tabianchi inaleta mafuriko na maji mengi yanatiririka, maradhi mengi yanatokea yasiyo ambukizwa ikiwemo kipindupindu. Serikali ina mpango gani kuweka mafunzo kila mahali ambayo yatadhibiti usafi na kuona kwamba, ni mwendelezo na tabianchi yetu? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza, nianze kwa kuwashukuru wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro, kwa sababu kwa kweli wametuletea mama yetu ambaye sisi Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro ni mama, ni dada na ni mshauri mzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nijibu maswali yake mawili; moja, hili la kwamba, wakati wa COVID tulikuwa kwa kweli na tabia nzuri ya kunawa mikono na kuzingatia usafi wetu kuanzia kunawa kwa maji, lakini kutumia sanitizer na vitu vingine. Mimi nitumie fursa hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote kwamba, hiyo tabia tuliyokuwa nayo mwanzo tuendelee nayo.

Mheshimiwa Spika, niombe, kwa sababu hapa Bungeni na sisi sasa tuwe wa mwanzo kwanza kurudisha hiyo tabia ndani ya Bunge haraka haraka. Wakati huko kwenye taasisi tukifanya mawasiliano kwa kushirikiana na wenzetu wa Wizara tofauti tofauti tuendelee na hiyo tabia kwa pamoja. Hiyo ni moja.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la kwamba, sasa hivi kuna mafuriko. Ni kweli mafuriko yanapokuwepo maji yanapokuwa yametuama kuna magonjwa mbalimbali ambukizo ambayo yanaenda kutokea ikiwepo malaria na mambo mengine. Nimhakikishie Mbunge kwamba, Serikali ipo macho kwa ajili hiyo ndiyo maana unaona vifo vya watoto kwenye eneo la malaria haviongezeki. Pia, husikii milipuko ya kipindupindu na vitu vingine pamoja na matatizo yote yanayotokea ambayo unayasikia sehemu mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikielekea upande huo na kuhakikisha inazingatia ushauri ambao umeusema. Ninachotaka kuhakikisha kutoka hapa Bungeni nitumie fursa hii kuwaomba wataalamu wetu kuanzia zahanati zetu, vituo vyetu vya afya na kila mahali tuongeze nguvu kwenye eneo kama ambavyo umeshauri tuendelee kuongeza nguvu na tusirudi nyuma. (Makofi)