Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tecla Mohamedi Ungele
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka huduma za Mifuko ya Jamii ngazi ya Wilaya na Tarafa ili kuwaondolea usumbufu Wastaafu kwenda kuhakikiwa Mkoani?
Supplementary Question 1
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Ni mkakati mzuri sana unaoendelea kuwahudumia wastaafu hawa. Ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Je, Serikali imejipangaje kutoa elimu ya uhakiki kwa ngazi za Halmashauri katika matumizi ya TEHAMA ili kurahisisha uhakiki huo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Katika majibu, nimesikia kwamba mikoa na baadhi ya wilaya huduma hizo zimekwenda, lakini kuna baadhi ya Wilaya bado huduma hizo za uhakiki hazijafika. Je, ni lini Serikali itapeleka huduma hizo kwenye baadhi ya wilaya zilizobaki?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Spika, nikijibu maswali ya Mheshimiwa Mama Tecla kama alivyouliza.
Mheshimiwa Spika, kwanza, utaratibu wa elimu unaotolewa na mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni endelevu, na tunatoa kwa makundi kwanza ya wafanyakazi katika taasisi za Serikali na wale wote wanaohusika au wadau wanaohusika kwenye mtiririko mzima unaohusiana na mafao ya wastaafu.
Mheshimiwa Spika, hivyo hivyo, kupitia mfumo huo wa kidigitali ambao tunao tumekuwa tukitoa elimu kwa wanachama wenyewe kuwapelekea message mbalimbali. Kwa hiyo, jambo hili linaendelea na tulikuwa tumeshafikia zaidi ya wanachama 16,000 ambao tunaendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili linafanana na la kwanza. Tumefanya hii kazi katika mikoa, wilaya na mamlaka nyingine zote za Serikali. Kama kuna wilaya mahsusi ambazo Mheshimiwa Mbunge anazo na anaamini kwamba hazijafikiwa katika utoaji wa elimu, namwomba Mheshimiwa aweze kunifikishia tu hapa mezani, nami mwenyewe kwanza kwa sababu ni mama yangu nitamfuata hapo ili niweze kuhakiki ofisini kama kweli hawajaweza kufikishiwa elimu, waweze kufanyiwa hivyo, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved