Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA K.n.y. MHE. MAIDA HAMADI ABDALLAH aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa madai ya muda mrefu Askari Polisi waliomaliza muda wao?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mwanana ya swali hili. Tumekuwa tukihimiza sana matumizi ya IT (mfumo wa kidijiti) kwa watumishi wote.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; je, ni kwa nini ripoti zisiwekwe vizuri ili mfumo huu urekodi mambo yote ya mahitaji anayotakiwa kulipwa askari mstaafu (mafao yake na kila kitu chake); badala ya ile siku ya mwisho anapomaliza kazi kumtaka athibitishe alianza lini, alipandishwa cheo lini na alikopa kitu gani, jambo ambalo linaleta usumbufu?

Mheshimiwa Spika, je, Serikali inatambua kwamba askari hawa wanayahitaji zaidi mafao hayo kuliko siku nyingine yoyote?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asha Juma kama iofuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Jeshi la Polisi lipo katika maboresho makubwa sana ya kuweka mfumo wa kielektroniki ili kuhakikisha kwamba taarifa zote za askari zinaingia kwenye mfumo huo ili kuepuka usumbufu wakati wanapomaliza muda wao wa kazi na kupata madai yao kwa muda. Ahsante sana.