Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: - Je, Serikali inatumia utaratibu gani wa kuratibu na kutekeleza ahadi za Viongozi Wakuu nchini ili zisionekane ni za uongo?
Supplementary Question 1
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali, majibu ambayo yanatia moyo na kuonyesha kwamba ni kweli kuna uratibu. Nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa sababu ahadi hizi huwa zinatekelezwa kwenye Wizara za Kisekta. Je, Serikali haioni umuhimu, huko kwenye Wizara za Kisekta kukawekwa mafungu maalumu, yaani kwenye bajeti ikaonekana kwamba fedha hizi zinakwenda kutekeleza ahadi fulani ili Wabunge waweze kufuatilia pale ambapo bajeti hiyo inaweza kutekelezwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kule kwangu barabara ya Nangurukuru – Liwale na Nachingwea – Liwale, ni miongoni mwa ahadi za Uchanguzi wa 2015/2020. Je, ni nini kauli ya Serikali juu ya utekelezaji wa ahadi hizo?
Name
Tunza Issa Malapo
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee kumpongeza Mheshimiwa Kuchauka kwa kazi, lakini nimwambie kwenye hili la Wizara za Kisekta, ahadi za viongozi ni kipaumbele cha kila sekta wanapowasilisha bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wamekuwa wakiendelea kuziweka kila wanavyowasilisha bajeti zao. Sisi Ofisi ya Waziri Mkuu, tunafanya kazi ya kuratibu kuhakikisha kwamba ahadi hizi zimewekwa na kama nilivyosema kwenye dashboard tunaona kila ahadi imefikia hatua gani na asilimia ngapi kwenye utekelezaji, kwenye kila sekta.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, Halmashauri ya Liwale kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI mwaka jana tu tumetoa fedha kwenye yale maafa yaliyotokea ya El Nino na Kimbunga Hidaya, shilingi bilioni 1.3 ili kuweza kuendelea kutengeneza barabara zile. Lakini pia, bajeti yako Mheshimiwa Mbunge Kuchauka imeongezeka kutoka shilingi milioni 839 hadi tunavyoongea leo ni shilingi bilioni 2.4. Nataka nikuhakikishie, ahadi zote za Viongozi wetu Wakuu tunaendelea kuzifanyia kazi. Sisi tunawaomba Watanzania waendelee kutuamini, waendelee kuiamini Serikali ya Awamu ya Sita, kwa sababu ahadi zote ni vipaumbele vya Serikali, ahsante. (Makofi)
Name
Charles John Mwijage
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: - Je, Serikali inatumia utaratibu gani wa kuratibu na kutekeleza ahadi za Viongozi Wakuu nchini ili zisionekane ni za uongo?
Supplementary Question 2
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini ahadi ya Waziri Mkuu ya kujenga Kituo cha Afya katika Kata ya Butimba itatekelezwa?
Name
Ummy Hamisi Nderiananga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba niagize Wizara ya Kisekta iendelee kulifanyia kazi jambo la Mheshimiwa Mbunge ambalo ameulizia kuhusu ujengaji wa kituo hicho cha afya.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved