Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kiwanja cha Ndege Mwanza watalipwa fidia zao kwa kuwa tathmini imefanyika mara mbili sasa?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Suala hili limechukua muda mrefu sana, wananchi wamekuwa wakipewa matumaini na wamefanyiwa uthamini mara mbili, lakini leo wakati wanasubiri kulipwa, bado wanaambiwa Serikali inajipanga tena kwa ajili ya kuwapa viwanja.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu. Kwa kuwa, Serikali inaonekana sasa imebadilisha mtazamo wa kuwalipa na badala yake inataka kuwapa viwanja vya bei nafuu, naomba kufahamu, ni lini mchakato huo utakwisha ili basi, wananchi waweze kuishi kwa amani?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa, wananchi wamezuiwa kuendeleza majengo yao na sasa mengi yameanza kubomoka kulingana na mvua inayoendelea, wakati huo huo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege haiwezi kufanya maendelezo yoyote kwa sababu, bado kuna interest ya third party ambayo Serikali haijailipa, je, Serikali haioni kwamba kuchelewa kuwalipa wananchi hawa ni kuchelewa pia kupandishwa kwa hadhi ya uwanja ule kuwa wa Kimataifa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwenye hili zoezi ambalo sasa tunakwenda kupima viwanja na kuwamilikisha hawa wananchi, haya yamekuwa ni maelekezo ambayo yanatakiwa yafanywe kwa haraka sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, watakaopewa viwanja hivi pamoja na wananchi wa Mwanza ni wale tu ambao wanatakiwa fidia, yaani wana haki ya kupata fidia kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo, ni suala ambalo tunategemea kwamba, tutalifanyia haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ucheleweshwaji, sheria zipo. Naamini kwamba, kama kuna wananchi watakuwa wana madai zaidi kwa maana ya kucheleweshewa, ndiyo maana sheria ipo. Nadhani Serikali tumekuwa tunalipa, pale tunapochelewa, tunawalipa riba yao. Kwa hiyo, nadhani utaratibu huo huo utatumika pia kwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa wananchi ambao watapata kadhia hii, ahsante.