Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rehema Juma Migilla
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuruhusu maeneo ya hifadhi yaliyokosa sifa yatumike kwa matumizi ya kilimo na makazi?
Supplementary Question 1
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Vijiji vya Mwanduti, Kipendamoyo Mashariki, Kasandalala, Imagi, Usinga na Kakoko vina GN ya Serikali na vimesajiliwa. Hata hivyo, mpaka dakika hii vinasemekana na vinaonekana viko kwenye hifadhi.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, ukweli ni kwamba, vijiji hivi vimeshakosa hadhi kuwa kwenye hifadhi kwa sababu, hakuna wanyama, misitu wala hakuna vyanzo vya maji kama mito na maziwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, wananchi wetu wanaendelea kuishi kwa tabu sana katika maeneo haya, wanasumbuliwa sana na watu wa maliasili na wanaishi maisha ya taabu ya kuhangaika. Je, pamoja na hayo majibu uliyosema, ni kwa nini Serikali haioni haja ya kuendelea kufanya upanuzi wa maeneo hayo na kuvirasimisha hivi vijiji viwe ni makazi ya wananchi na wafanye shughuli za kibinadamu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuongozana nami kwenda jimboni kwangu ili akajionee hali halisi ya hivi vijiji na ashuhudie haya ninayoyaongea?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja ni maeneo ambayo yapo chini ya Wakala wa Usimamizi wa Huduma za Misitu Tanzania. Maeneo haya ni ardhi oevu, ambayo ni bakuli la kukinga maji ambayo yanaingia Mto Malagarasi na hatimaye Ziwa Tanganyika.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili ni muhimu sana kwa ikolojia ya eneo lile na uhifadhi katika nchi yetu. Namwomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuwa na subira wakati Serikali inaangalia jinsi ambavyo kwanza itarejesha yale ambayo yamepoteza hadhi kurejeshewa hadhi yake na pale itakapoonekana kuna uhitaji wa kuyamega maeneo hayo, basi mchakato wa kawaida ndani ya Serikali utafanyika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, niko tayari kuongozana naye kwenda kwenye maeneo hayo.
Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuruhusu maeneo ya hifadhi yaliyokosa sifa yatumike kwa matumizi ya kilimo na makazi?
Supplementary Question 2
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, Hifadhi ya Wamimbiki ina mgogoro wa muda mrefu wa mipaka na vijiji vitano ambavyo ni Kanga, Kaole, Kunke, Muhumbilo na Kidudwe. Pia, kwa kuwa, Mheshimiwa Rais kupitia timu ya Mawaziri nane ameridhia kutoa hekta 7,500. Je, Wizara ya Maliasili mko tayari kushirikiana na Wizara ya Ardhi kwenda kupima na kuwapa wananchi haya maeneo na kuondoa huu mgogoro? Ahsante.
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikifanya jambo hili na timu ya kushughulikia jambo hili chini ya uongozi wa mkoa, iko uwandani na inaendelea na kazi. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na subira, ndani ya muda mfupi jambo hili litakamilika.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved