Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga vituo vya Polisi Tarafa za Daudi na Nambis Wilayani Mbulu?

Supplementary Question 1

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Kituo cha Polisi katika Wilaya ya Mbulu ni chakavu na kilijengwa muda mrefu miaka ya zamani. Je, Serikali ina mkakati gani wa ujenzi wa Kituo cha Polisi katika Wilaya ya Mbulu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa makazi ya polisi katika Wilaya ya Mbulu yamechakaa sana hadi sasa. Je, Serikali ina utaratibu gani wa kukarabati makazi ya polisi nchi nzima ikiwemo Wilaya ya Mbulu?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Issaay, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, Wizara kupitia Jeshi la Polisi itafanya tathmini ya uchakavu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mbulu pamoja na makazi ya askari ili kujua gharama inayohitajika na hatimaye kupanga kwenye mpango na kupangia bajeti tayari kwa ajili ya ukarabati. Ahsante sana. (Makofi)