Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anton Albert Mwantona

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Primary Question

MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Taasisi zinazohudumia watu wengi zinaweka mifumo ya majiko ya gesi ili kuokoa mazingira?

Supplementary Question 1

MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niipongeze Serikali kwa kuweka ruzuku kwenye majiko ya gesi. Wamesema wameweka bilioni 8.64 na majiko zaidi ya laki nne na hamsini na mbili yamekwishagawiwa, hiyo ni hatua mojawapo nzuri zaidi. Pia kwenye jimbo langu nimeshapata majiko zaidi ya 1,600, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; hizi taasisi zinatumia kuni nyingi sana, maelfu ya tani kwa mwaka. Sasa, ninaona, kwa sababu wamekwishaweka ruzuku kwa watumiaji wadogo wadogowadogo. Je, Serikali ina mpango gani kuweka ruzuku kwenye taasisi hizi kubwa hasa kwenye ujenzi wa miundombinu ili majibu haya yasaidie ku-save mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Rungwe kuna mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, wameanzisha mradi pale wa kutengeneza mkaa kwa matumizi ya nyumbani. Je, Serikali itakuwa tayari kwenda kutembelea huu mradi kwa lengo la kusaidia uzalishaji uwe mkubwa zaidi na bei ya makaa iweze kupungua kwa sababu sasa hivi wanauza kilo moja kwa shilingi 1,000 kiasi kwamba wananchi wengi hawawezi ku-afford hiyo bei?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Anton Albert Mwantona, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali tayari imeshatoa maelekezo ya taasisi zote zinazolisha watu zaidi ya 100 kwa siku zitumie nishati safi ya kupikia na kwa kuwa Serikali hiyo hiyo, tayari imeshatoa maelekezo ya wananchi Tanzania nzima tufanye jitihada katika kupanda ili tunusuru mazingira yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, kwa kuwa Serikali imeshaanza hatua za kufanya punguzo, angalau wananchi waweze ku-afford matumizi ya nishati safi ya kupikia, nimwambie tu kwamba Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na Wizara ya Nishati tuko katika hatua ya mwisho kuhakikisha kwamba tunakamilisha utaratibu wa kukamilisha uwepo wa Mfuko wa Nishati ambao unaitwa CookFund.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfuko huu utawezesha mtu mmoja mmoja, taasisi, kampuni hata vikundi vya watu. Lengo na madhumuni kuweza ku-afford matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tayari Serikali imekwishaandaa mkakati wa miaka 10 kuanzia 2024 mpaka 2034 kwa ajili kuhakikisha kwamba kwanza wananchi wanaweza kuhimili matumizi ya nishati safi ya kupikia na kusaidia kuendelea kutoa elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa siyo mkaa wa mawe tu, lakini hata makaa mengine hapa, ambao ni mkaa mbadala ikiwemo mikaa ya kutumia miti, majani, makaratasi na hata vinyesi vya wanyama, nimwambie tuko tayari na tutapanga muda wa kwenda kutembelea katika mgodi huo ili kuendelea kuwaelimisha wananchi na pia kuendelea kujaribu kukaa na taasisi mbalimbali kuona namna ambavyo tunaweza tukashauri kama Serikali kuweza kupunguza hizo gharama za upatikanaji wa huu mkaa.