Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza:- Je, lini Wananchi wa Kata za Kasamwa na Nyamkumbu - Geita Mjini watalipwa fidia kutokana na alama za barabara kuwekwa katika maeneno yao?

Supplementary Question 1

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri ingawa majibu haya pia niliyapata miaka mitatu iliyopita na sijajua zoezi litakamilika lini. Ninaomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Sheria ya Fidia inatoa fidia kulipia maendelezo ambayo yamekutwa pale site, kwa sababu muda unakuwa mwingi, assest zilizopo zinabomoka na zinapotea. Je, Waziri haoni kwamba wakati Serikali inakamilisha uchunguzi itakuta maeneo yale tayari yameshakuwa wazi na hivyo yatakuwa hayana thamani ya mwanzo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Barabara ya kutoka Mwanza kwenda Bukoba ambayo inapita katikati ya Mji wa Geita ilijengwa bila mitaro. Kwa hiyo, kila mvua inaponyesha inasababisha mafuriko kwenye Mji wa Geita. Je, ni lini Wizara itawapatia TANROADS fedha waweze kuweka mitaro kwenye Mji wa Geita? Nakushukuru sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Fidia iko wazi sana, pale ambapo inakuwa imepita miezi sita tunalipa riba, kwa miaka miwili maana yake lazima turudie kufanya tathmini ya ulipaji wa fidia. Hili litafanyika kama itaonekana kwamba kwenye hili eneo hawa watu wanatakiwa kulipwa fidia na kuondolewa ili kupisha ujenzi. Hii ni sambamba na maeneo yote katika nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, siyo mara ya kwanza, aliliuliza na ameliuliza tena. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunavyoongea sasa hivi tulishatenga fedha na tumeshampata mkandarasi; na utekelezaji wa kutengeneza mitaro upya katika Mji wa Geita likiwepo lile eneo la karibu na stendi, mkataba uko kwa mwanasheria ili mkandarasi huyo aanze utekelezaji katika mwaka huu wa bajeti tunaoendelea nao.