Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali yanayotia moyo kwani wahenga wanasema, usiposhukuru kwa kidogo huwezi kushukuru kwa kingi na asiye na shukrani ya kumshukuru mwanadamu mwenzie basi hata Mwenyezi Mungu hawezi kumshukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; iko Barabara ya Morogoro inayounganishwa na Mkoa wa Lindi kupitia Wilaya ya Liwale – Mahenge – Kilombero mpaka hapa Dodoma, ambayo ni barabara fupi sana iwe backup ya barabara hii ambayo sasa inatusumbua badala ya hiyo route wanayotuambia ya kwenda Njombe – Iringa mpaka Songea. Hiyo route ingekuwa ni fupi sana kwa kuja Dodoma kwa sababu ni barabara inayotoka Mahenge – Kilombero – Dumila uko Dodoma. Je, ni nini mpango wa Serikali kuijenga barabara hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; iko Barabara ya EPC+F kilometa 175 kutoka Masasi mpaka Liwale kupitia Nachingwea ni mwaka wa tatu sasa tangu tumesaini mikataba ya barabara hiyo. Je, nini mpango wa Serikali wa kuijenga barabara hiyo? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na swali la kwanza la Mheshimiwa Kuchauka, ni kweli kwamba upo mpango wa kufanya upembuzi yakinifu kwa barabara ya Liwale kwenda Ulanga, barabara hii inapita kwenye Mbuga ya Selous. Kwa hiyo, Wizara ya Ujenzi kwa kusaidiana na wadau wengine, tulishatenga ipo kwenye mpango na tulishatenga bajeti kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu kwa sababu ni barabara ambayo inapita kwenye mbuga, kwa hiyo kuna wadau wengi ambao wanahusika katika kufanya hivyo. Once tukishakamilisha, tutakuwa tayari kuanza kuijenga hiyo barabara kati ya Mkoa wa Lindi na Morogoro kuja Dodoma ambayo itakuwa ni fupi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili ambalo ni la Barabara kilometa 175 ya Liwale – Nachingwea – Masasi, tulishaeleza kwamba ule mpango wa EPC+F baada ya kuachana nao tunakwenda sasa kwenye sanifu jenga na hizi barabara zimewekwa kwenye vipande. Katika hii barabara tutaanza kujenga kilometa 55 ambayo tutaanza kutokea Liwale hadi eneo linaitwa Kiangala na tunavyoongea tayari tumeshasaini mkataba. Mkandarasi ni yuleyule ambaye tulikuwa naye awali, kwa hiyo, tunategemea baada ya taratibu zote kukamilika tutaanza kujenga hiyo barabara ya kilometa 55 tukianzia Liwale. Ahsante. (Makofi)

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 2

MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Mtwara – Kibiti – Lindi ni barabara ambayo sasa imeshakuwa kongwe na ilijengwa huko nyuma ndani ya miaka kama 40 iliyopita. Ninamshukuru Mheshimiwa Rais ameshatoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja. Je, ni lini sasa ujenzi huu wa madaraja utakamilika kwa sababu imekuwa sasa kila tunapozungumza tunaambiwa upembuzi yakinifu, upembuzi yakinifu! Tunaiomba Serikali itueleze ni lini madaraja yale yatajengwa na lini yataisha? Ninakushukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli barabara hii ni kongwe na sasa hivi imekuwa ni kati ya barabara moja ambayo inapitisha magari mengi sana makubwa na mazito. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, baada ya mafuriko ya mwaka jana, Mheshimiwa Rais alitafuta fedha na ni fedha ambazo katika madaraja yote ya hii Barabara ya Kibiti – Lindi yapo kwenye mpango, wakandarasi tulishawapata, kazi za kuyajenga madaraja yote zimeanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ufanisi ambao umefanyika ni kulingana na ukubwa wa matokeo tuliyoyaona mwaka jana. Kwa hiyo, madaraja yote yanapanuliwa na tulishapata wakandarasi kwenye barabara hiyo yote ambapo wameshaanza kazi ya kuyajenga hayo madaraja. Ahsante.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 3

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Barabara ya kutoka Somanga – Nangurukuru hadi Mbwemkuru imekuwa ikisumbua sana na hadi wakati huu kuna changamoto kubwa sana kule. Je, Serikali ina mkakati gani madhubuti wa kuhakikisha hiyo barabara haikatiki mara kwa mara?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu swali la Mheshimiwa Mtenga; maeneo mengi yaliyokatika ni yale ambayo mito inapita ama kuna mabonde. Maeneo yote hayo ambayo tuliwaonesha mwaka jana, yote yametengewa fedha za dharura na tunavyoongea sasa hivi tumeshapata wakandarasi ambao wameanza kazi na tunajua itakuwa ni tiba ya kudumu. Ahsante.

Name

Ndaisaba George Ruhoro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 4

MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Wananchi wa Tarafa za Rulenge na Murusagamba wanafahamu kwamba, Barabara yao ya Murugarama – Rulenge hadi Nyakahura ina mkandarasi na wanafahamu mkandarasi ameomba advance payment zaidi ya mwaka mmoja uliopita, hajalipwa. Ni upi mkakati wa Wizara ya Ujenzi kuhakikisha mkandarasi analipwa advance payment, ili barabara ya wananchi hawa ianze kujengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge wa Ngara, barabara hii tayari mkandarasi ameshapatikana na sisi, kama Wizara ya Ujenzi, tumeshakamilisha taratibu zote, tumeshawasilisha maombi ya mkandarasi kwa Wizara ya Fedha na tayari tumeshaanza kulipa advance payment nyingi sana kwenye barabara. Ninaamini muda si mrefu tutamlipa huyo mkandarasi, ili aweze kuanza kufanya hiyo kazi ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Amandus Julius Chinguile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nachingwea

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 5

MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Barabara ya Nachingwea – Mkotokuyana na Nanganga ni muhimu kwa uchumi wa Nachingwea na pia, kimawasiliano kuelekea makao makuu ya mkoa. Ni lini Serikali itaijenga barabara hii kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nikiri kwamba, hii barabara ipo kwenye mpango, ni barabara ambayo haizidi kilometa 45 na tayari tumeshakamilisha usanifu. Tunachofanya sasa hivi katika mpango wa mwaka ujao ni tunaamini, tutaanza kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 6

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Barabara ya Newala kuelekea Mbuyuni ilikuwa katika utekelezaji wa upembuzi yakinifu. Je, suala hili limefikia wapi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tulishaiweka kwenye mpango na taratibu za kukamilisha huo upembuzi yakinifu zinaendelea. Ahsante.

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 7

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, leo naongea polepole. Mheshimiwa Waziri aliniahidi kwamba, upembuzi yakinifu ama mshauri elekezi, kwa ajili ya ujenzi wa Barabara yetu kwa kiwango cha lami kutoka Kahama – Nyang’hwale kwenda Busisi, mkandarasi huyu atamtangaza mwezi Februari na leo ni mwezi Aprili na ninasimama kila mara hapa, ama anataka niruke sarakasi? Ninaomba majibu sahihi kabisa leo. Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimwombe kaka yangu Mheshimiwa Amar kwamba, kazi hizi za upembuzi yakinifu zinapofanyika wakati fulani unaweza usiwaone. Nimwombe baada ya kipindi hiki mimi na yeye, Mheshimiwa Mbunge, tuweze kuongea pamoja tuone changamoto itakuwa ni nini? Maana hii inasimamiwa na makao makuu kwa sababu, ni barabara ambayo inaunganisha mikoa takribani mitatu. Ahsante.

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa Km 231 utaanza?

Supplementary Question 8

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini ujenzi wa Barabara ya kutoka Rangi Tatu – Kokoto – Kongowe utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, hii barabara tutakachoanza kwanza ni kujenga daraja, lakini mpango tumeshauweka; Mheshimiwa Mbunge anafahamu kwamba, tumeshapanga. Tunachotegemea sasa hivi ni kupata advance payment ili mkandarasi aanze kujenga hiyo barabara. Ahsante.