Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano Vijiji vya Lukani na Ng’uluhe - Kilolo ili kuboresha mawasiliano?

Supplementary Question 1

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri na pia ninaishukuru Serikali kwa kukamilisha minara katika Kata zilizotajwa za Ilole na Masisiwe na mawasiliano yanaendelea vizuri, lakini nina maswali yangu mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; mnara unaojengwa katika Kata ya Kimala ulisimamishwa kutokana na mgogoro kati ya TFS na wajenga mnara kwamba wamejenga kwenye eneo la msitu. Je, Serikali haioni ni wakati muafaka wa kutatua mgogoro huo ili mnara ule uweze kukamilika na wananchi wa Kata ya Kimala waweze kupata huduma?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; minara mitatu ya maeneo ya Kata ya Mahenge, Ibumu na Uhambingeto imekuwa ikijengwa, lakini kwa kasi ndogo sana. Je, Serikali kwa kuzingatia kwamba uchaguzi unakaribia na baadhi ya kura zinategemea minara hiyo haioni sasa ni wakati muafaka wa kukamilisha minara hiyo ili kufanya mawasiliano mazuri na wajumbe wakati tukiomba kura?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

Mheshimiwa Naibu Spika, nikupongeze sana Mheshimiwa Justin Nyamoga kwa kazi nzuri ambayo unaifanya na tunashukuru kwa appreciation kwa maeneo ambayo tayari tumeweza kukufikia. Nikutoe hofu migogoro yote ambayo inatokea katika utekelezaji wa ujenzi wa minara tunaishughulikia na huu pia ninaomba niseme nimeupokea na nitausimamia kwa karibu kuhakikisha kwamba unakamilika ili ujenzi wa mnara uweze kufanyika na wananchi wapate huduma ya mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika minara hii mitatu, kwamba kasi yake ni ndogo; Mheshimiwa Mbunge, Kaka yangu Mheshimiwa Nyamoga nikutoe hofu kuwa Mheshimiwa Waziri, Jerry Silaa ameshatoa maagizo minara hii yote inatakiwa ikamilike ndani ya muda ambao mkataba umesainiwa hivyo SPID wameshaagizwa na sasa hivi utaona mabadiliko makubwa katika ujenzi wa minara hii na hata namna ya kuelekeza wananchi wakati wa uchaguzi itakuwa nyepesi kwako, lakini vilevile kwa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. (Makofi)

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano Vijiji vya Lukani na Ng’uluhe - Kilolo ili kuboresha mawasiliano?

Supplementary Question 2

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano katika vijiji vya Mkoa wa Simiyu ambavyo havina mawasiliano? (Makofi

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Midimu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo aliyoyataja tuna minara ambayo tayari ipo kwenye Mradi wa Tanzania ya Kidigitali, minara 758 lakini tuna minara 632. Kwa hiyo, tunatarajia kuyafikia maeneo yote ya Tanzania na bado tuna batch nyingine ya minara ambayo TTCL pia watakuja kuijenga. Hivyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Esther Midimu maeneo hayo ya vijiji vyote alivyovitaja tutakuja kutekeleza ujenzi wa minara. (Makofi

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano Vijiji vya Lukani na Ng’uluhe - Kilolo ili kuboresha mawasiliano?

Supplementary Question 3

MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itajenga mnara katika Kata ya Mabalanga, Jimbo la Kilindi ambapo kuna mradi mkubwa wa Serikali wa shule kubwa ya kisasa ya wasichana? Ninashukuru. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zodo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya Kilindi tena kwenye ujenzi wa sekondari maeneo yote yanayotoa huduma za umma ni kipaumbele chetu kuhakikisha mawasiliano yanaimarika tena si tu 2G tunasisitiza 3G, 4G kwa sababu vijana wetu sasa wanasoma pia kidigiti. Kwa hiyo, eneo hili pia Mheshimiwa Mbunge nimelichukua kuhakikisha kwamba wataalam wetu wanafika na kazi ya ujenzi wa mnara iweze kupangiwa muda wake. (Makofi)

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano Vijiji vya Lukani na Ng’uluhe - Kilolo ili kuboresha mawasiliano?

Supplementary Question 4

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri mwaka jana alitembelea Jimbo la Ukerewe, Kata ya Bukiko na kupitia mnara wa Halotel. Eneo lote lile la Kata ya Bukiko lina shida kubwa ya mawasiliano na kuna maelekezo alitoa. Kuna shida gani watendaji kutekeleza maelekezo aliyoyatoa tukawaondolea tabu wananchi wa Kata ya Bukiko wenye shida kubwa ya mawasiliano? Kwa sababu mpaka sasa hakuna mawasiliano kwenye Kata nzima ile ya Bukiko. Mheshimiwa Naibu Waziri ninaomba msaada wako na ninaomba maelezo kwenye hili. Ninakushukuru.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph, Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mimi na yeye tulitembelea eneo la mradi na ule mnara kwa taarifa nilizonazo Halotel wameweza ku-upgrade. Kwa hiyo, ninafikiri tu ni kazi ya kiufundi kidogo labda ku-twist kidogo hivi ili kuona kwamba uelekeo wake sasa usababishe mawasiliano ya uhakika katika Kata ya Bukiko. Ninaomba nipokee na nitasimamia maelekezo niliyoyaacha Kata ya Bukiko. (Makofi)

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga minara ya mawasiliano Vijiji vya Lukani na Ng’uluhe - Kilolo ili kuboresha mawasiliano?

Supplementary Question 5

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kata ya Napacho iliyopo ndani ya jimbo langu Mkandarasi Minara Tanzania alipewa kazi ya kusimika minara katika jimbo langu, sasa ni mwaka mmoja umepita tangu mkandarasi huyo aripoti ndani ya eneo na kutoweka. Nini kauli ya Serikali juu ya Mkandarasi huyu? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mhata kwa ufuatiliaji wa ujenzi wa minara ya mawasiliano katika Kata hii ya Napacho, ninaomba nipokee na nimwagize Meneja anayehusika na kanda ile ya kusini kuhakikisha anafahamu kwa nini Mnara Tanzania hajaja kutekeleza mradi huu na ikibidi sheria iweze kufuata mkondo wake kwa sababu ameshasaini mkataba; basi tuweze kuona namna ya kumpatia mtoa huduma mwingine ambaye atatuletea mnara maeneo haya ya Napacho na mawasiliano kuimarika. (Makofi)