Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa utaanza Mkoani Njombe?

Supplementary Question 1

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote ninashukuru sana kwa hatua iliyofikiwa na maelezo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameyatoa. Kwa namna ya pekee tunashukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu hii ilikuwa ni ahadi aliyoitoa kwa Wana-Njombe alipotutembelea mwaka 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali moja la nyongeza. Kwa vile Mji wa Njombe unakua kwa haraka na sasa mapendekezo ya kuwa manispaa yana ngoja maamuzi ya Serikali na kwa vile pressure ya ardhi katika Mji wa Njombe ni kubwa sana, eneo hilo lipo katikati kabisa ya mji. Je, Serikali inaweza kufikiria kulirudisha eneo hilo kwa halmashauri yetu ya mji ili tuweze sasa kufanya matumizi mengine ambayo ni ya muhimu sana kwa shughuli za kijamii? (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Deo Mwanyika kwa ufuatiliaji wake wa karibu wa Uwanja wa Ndege wa Njombe ambao kama nilivyoeleza ni muhimu sana kwa maslahi ya mkoa huo na maeneo ya nyanda za juu kusini kwa ujumla. Pili, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa Mnyaa nipokee shukrani alizozitoa kwa Serikali ya Awamu ya Sita ambayo inaahidi na kutekeleza. Hoja yake ya mwisho amezungumzia kuhusiana na kuomba eneo hilo ambapo tutakapohamisha uwanja kama lingeweza kutumika kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Njombe.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana Bunge lako Tukufu lilipitisha Sheria Namba 108 ya mwaka 2024 ambayo pamoja na mambo mengine imetoa mwongozo wa namna ya kufanya uendelezaji wa rasilimali za viwanja vya ndege nchini. Hivyo, mara baada utakapokamilisha uhamishaji wa kiwanja hicho Mamlaka ya Viwanja vya Ndege itaweka mfumo mzuri wa kukaribisha wawekezaji wa ndani na wa nje ikiwemo mwananchi mmoja mmoja pamoja na halmashauri hivyo, nitamwomba na yeye Mheshimiwa Mwanyika pamoja na halmashauri muda ukifika basi waweze kuchangamkia fursa hiyo ili kuendeleza eneo hilo kwa maslahi ya wananchi na nchi yetu.

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa utaanza Mkoani Njombe?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Uwanja wa Ndege wa Bukoba unaweza uka-accommodate ndege ndogo, lakini tuna abiria wengi sana. Ni lini sasa Serikali itajenga uwanja mkubwa na wa kisasa wa kimataifa wa Bukoba? (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa Mkoa wa Kagera kuwa na uwanja mkubwa ambao utaweza kuendana na mahitaji ya sasa. Awali tulipanga kufanya maboresho katika uwanja ule uliopo ikiwa ni pamoja na kujenga jengo la kuongozea ndege pamoja na kuweka taa, lakini baada ya kubaini umuhimu mkubwa Serikali imeanza mchakato wa kutafuta eneo lingine. Tayari eneo limeshapatikana tumeanza taratibu za awali ili kujenga uwanja mkubwa ambao utakuwa ni wa kisasa na utaweza kusaidia shughuli mbalimbali za Mkoa wa Kagera na wilaya zake.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa utaanza Mkoani Njombe?

Supplementary Question 3

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo la nyongeza. Uwanja wa Ndege wa Musoma umekuwa ukipewa ahadi kwa muda mrefu kukamilika kwa kiwango cha lami na kama mnavyojua Mkoa wa Mara ni mkoa ambao umeshiriki katika harakati za nchi hii, anakotokea Baba wa Taifa, ili kumuenzi ni lini watakamilisha Uwanja wa Ndege wa Musoma kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Musoma siyo tu kama alivyozungumza Mheshimiwa Mbunge kwa maana kama kumuenzi Baba wa Taifa, lakini pia huko ndiko kuna utalii kwa wingi lakini shughuli za madini pamoja na shughuli za uvuvi. Hivyo basi, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunaendelea na mchakato wa kukamilisha taratibu za ndani kwa maana ya kuwalipa wakandarasi ili ujenzi huo sasa uweze kuendelea na ninakuhakikishia kwamba utakamilika na utakwenda kuwanufaisha wananchi wa mkoa huo.