Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Lake Oil - Ijuganyodo hadi Kyamunene itajengwa kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Spika, ahsante, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali madogo mawili.
Mheshimiwa Spika, barabara hii ni ya kimkakati kwa Manispaa yetu ya Bukoba inaenda kwa mwekezaji mkubwa wa shule ambazo zinafanya vizuri kitaifa za Kaizirege na Kemebos na yeye amekuwa akishirikiana na Serikali kutengeneza barabara hii. Sasa ninaomba commitment ya Serikali kwamba ni lini itawekewa lami ili iendelee kuhudumia vizuri mwekezaji huyu, lakini na wakazi wengine wa maeneo hayo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, nilimwomba juzi Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kwamba Mradi wa TACTIC utakapokamilika basi usainiwe pale Bukoba Mjini ili Wana-Bukoba Mjini waweze kuona kwamba jambo hili linaanza kufanyika. Sasa ninaomba kujua ni lini mradi huo utasainiwa ili barabara zaidi ya kilometa 10 ziweze kutekelezwa katika Jimbo la Bukoba Mjini? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake ambayo nia ya kimsingi anataka kuona miundombinu ya barabara inaboreshwa katika jimbo lake. Kuhusiana na swali lake la mwanzo kama nilivyotangulia kujibu katika majibu ya msingi kwamba barabara hii ya Lake Oil - Ijuganyodo ipo katika mpango wa kufanyiwa ukarabati lakini lengo na nia ni kuijenga barabara hii katika hadhi ya lami.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika kipindi cha miaka minne tayari katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba jumla ya shilingi bilioni 9.6 zimewekezwa kwa ajili ya kukarabati na kujenga barabara za lami na mtandao wa lami umeongezeka kutoka kilometa 34.29 mpaka sasa mtandao wa lami ni kilometa 43.54. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kuongeza mtandao huu wa lami na itaifikia barabara hii muhimu kabisa ya Lake Oil – Ijuganyodo.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili Mheshimiwa Mbunge ameulizia kuhusiana na utekelezaji wa Mradi wa TACTIC, ni kweli Manispaa ya Bukoba Mjini na yenyewe ni miongoni mwa miji 45 ambayo inanufaika na Mradi huu wa TACTIC. Kwa awamu hii au kwa wakati huu tuliokuwa nao tayari mradi wa ujenzi wa barabara kilometa 10 katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge unaendelea na evaluation na tunatarajia mwezi Mei tutasaini mikataba ili mkandarasi sasa aweze kukabidhiwa site na aanze ujenzi.
Kwa hiyo, ninamwomba Mheshimiwa Mbunge yeye na wananchi wake wa Manispaa ya Bukoba Mjini wakae mkao wa mapokeo, barabara hizi zinakuja kujengwa kupitia Mradi wa TATIC pamoja na miundombinu mingine ya soko na stendi. (Makofi)
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Lake Oil - Ijuganyodo hadi Kyamunene itajengwa kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 2
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa barabara ya kutoka Kahama - Nyang’olongo – Bukwimba - Kharumwa mpaka Busolwa magari makubwa na mazito yameharibu barabara hiyo. Je, Serikali itapeleka lini fedha kwa ajili ya kufanya matengenezo ya kawaida?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, katika Serikali ya Awamu ya Sita bajeti ya TARURA imeongezeka maradufu kutoka bajeti ya shilingi bilioni 275 kwa mwaka mpaka sasa bajeti ya TARURA imefikia shilingi bilioni 710. Lengo ni kufikia mtandao mkubwa zaidi wa barabra hizi ambazo zinahudumiwa na TARURA.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunatambua umuhimu mkubwa wa barabara aliyoitaja hasa kiuchumi, lakini kwa kuwasaidia wananchi kufikia huduma za kijamii. Nimhakikishie kuwa Serikali itafika kuja kutengeneza barabara hii.
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Lake Oil - Ijuganyodo hadi Kyamunene itajengwa kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Ujenzi wa Barabara ya Akeri hadi Ndoombo kwa kiwango cha lami umesimama sasa hivi kwa takribani mwaka mmoja na nusu; je, ni lini Serikali inakwenda kupeleka pesa sasa hivi kwa ajili ya kumaliza hiyo kazi?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Pallangyo, amekuwa akifuatilia kwa ukaribu sana kuhakikisha katika jimbo lake miundombinu ya barabara hizi zinazohudumiwa na TARURA zinaweza kujengwa ziwe kwenye hadhi nzuri na kuweza kuwasaidia wananchi wake.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tutaendelea kufuatilia ili kuhakikisha mradi huu kama kuna changamoto yoyote unakwamuliwa ili uweze kuendelea na uweze kukamilika na uweze kuwanufaisha wananchi wako.
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza: - Je, lini Barabara ya Lake Oil - Ijuganyodo hadi Kyamunene itajengwa kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 4
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana, kwa kuwa Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya barabara mbili kutoka Clock Tower kuja YMCA na kwa kuwa Barabara ya Arusha nayo imeshafikia hatua ya utangazaji kwa ajili ya double road. Je, ni lini Serikali itazirejesha fedha kwa ajili ya double road kutoka YMCA mpaka KCMC ambazo zilisombwa kutokana na mafuriko yaliyotokea na hiyo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais? (Makofi)
Name
Yussuf Kaiza Makame
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Chake Chake
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri na niendelee kumhakikishia kwamba ahadi za viongozi wakuu ni kipaumbele namba moja katika mipango ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali. Ninaomba nimhakikishie kwamba Serikali tutafuatilia kuhakikisha kwamba barabara hizi alizozitaja zinaweza kupatiwa fedha na zinaweza kujengwa ziwe katika hadhi nzuri ili ziweze kuwanufaisha wananchi wake.