Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kulipa madeni ya wazabuni hasa ya Polisi na Magereza?
Supplementary Question 1
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wazabuni ambao mali zao zinauzwa na benki na wanafilisika? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kuna juhudi gani mahsusi za kulipa madeni haya makubwa ambayo wazabuni wanaidai Serikali? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Almas Maige, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, katika swali la kwanza namna ya kuwasaidia wazabuni. Ni kweli tunatambua kwamba wazabuni wanafanya kazi kubwa ya kutoa huduma katika taasisi mbalimbali za Serikali mbalimbali ikiwepo Majeshi yetu ya Polisi na Magereza. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itaongeza kasi ya uhakiki wa madeni haya ili kuweza kulipa kwa wakati na kuepukana na adha ya kuuziwa bidhaa zao na benki.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, juhudi za Serikali kama nilivyosema ni kuongeza kasi ya uhakiki wa madeni ili kuwalipa kwa wakati na kuondokana na adha hii kama nilivyosema kwenye jibu la msingi. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Rehema Juma Migilla
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kulipa madeni ya wazabuni hasa ya Polisi na Magereza?
Supplementary Question 2
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, Kata ya Uyowa na Kata ya Kona Nne hazina vituo vya polisi, hivyo shughuli za kipolisi zinafanyika kwenye nyumba za kupanga. Hali hiyo imesababisha wapangishaji kulidai Jeshi la Polisi fedha nyingi sana. Je, upi mpango wa Serikali kuhakikisha inatujengea vituo vya polisi ili kuepukana na kulipa madeni makubwa? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Rehema Migilla, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kujenga vituo vya polisi kwenye Kata zote hapa nchini pamoja na shehia kwa upande wa Zanzibar, vituo hivyo vitajengwa awamu kwa awamu. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge Kata zake alizozitaja pia zitaingizwa kwenye mpango na kutengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kulipa madeni ya wazabuni hasa ya Polisi na Magereza?
Supplementary Question 3
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, Askari wa Jeshi la Magereza wengine ni wastaafu na wengine bado wapo kazini wanadai madeni ambayo ni malimbikizo ya muda mrefu tangu 2010 ya safari za kikazi, uhamisho na mengineyo.
Mheshimiwa Spika, ninataka kujua ni lini Serikali itahakikisha inawalipa Askari hawa madeni yao? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Askari wetu wanaostaafu na wanaopata safari za kikazi wamekuwa wakilipwa madai yao na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, hata hawa ambao anawasema baadaye tuwasiliane, kama kuna Askari ambao wanadai madeni tutawasiliana kwa ajili ya kuwatengea fedha kuwalipa stahiki zao. (Makofi)
Name
Stanslaus Shing'oma Mabula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyamagana
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kulipa madeni ya wazabuni hasa ya Polisi na Magereza?
Supplementary Question 4
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, nataka kumuuliza Mheshimiwa Waziri ni lini fedha za kukamilisha Kituo cha Polisi Nyegezi zitapelekwa, lakini nimegundua swali la msingi halihusiani na ujenzi wa vituo vya polisi. Ninakushukuru. (Makofi/Kicheko)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Stanslaus Mabula, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli nilifika Kituo cha Polisi cha Nyegezi kule Mwanza na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tayari tumeshakichukua tumekiweka kwenye mpango tutakitengea fedha kwa ajili ya kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na wananchi wa Jimbo lake. Ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa iliyofanyika. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kulipa madeni ya wazabuni hasa ya Polisi na Magereza?
Supplementary Question 5
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, mbali ya kwamba Jeshi la Magereza na Polisi wanadaiwa na wazabuni, lakini pia Jeshi la Polisi Askari wake wamekuwa wakidai madeni mbalimbali ya uhamisho na wengine ambao wamestaafu bado hawajalipwa malipo ya mizigo na madeni mengine wakiwepo na Askari wa Bunda. Sasa, ni lini mtawalipa, maana tunao wajibu kwa kuwatetea hata kama wanatukamata na kutupiga virungu. Ninakushukuru. (Makofi/Kicheko)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli wapo baadhi ya Askari ambao wanadai fedha zao za uhamisho pamoja na mizigo kama ambavyo amesema. Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka na tumekuwa tukiendelea kuwalipa askari wetu kila mwaka kila mwaka. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba hata hawa wanaodai pia bado tutawatengea fedha na watalipwa wakiwemo Askari wa Jimbo la Bunda, ahsante. (Makofi)