Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme wa REA kwa vitongoji ambavyo bado havijapatiwa umeme wa REA Mbogwe?
Supplementary Question 1
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; ninafahamu mpango wa Serikali ni kutuwekea Substation Mbogwe ili kuondoa hali ya kukatika umeme kwenye wilaya hiyo. Je, lini sasa itaanza kujengwa hiyo substation?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Kata ya Nanda, Masumbwe, Nyakafuru na Lugunga transformer zilishazidiwa na haya maeneo yana viwanda vya mchele. Kila wakati mashine zinapowashwa umeme unakosa nguvu. Lini sasa katika maeneo haya Serikali itatubadilishia transformer ili wananchi wa maeneo yale waweze kufanya shughuli zao? (Makofi)
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge. La kwanza, kuhusiana na substation (kituo cha kupoza umeme) ya Mbogwe; Serikali inao mkakati wa kujenga kituo cha kupoza umeme pale Bukombe, kwa ajili ya majimbo mawili, Bukombe na Mbogwe na vilevile, kujenga line ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Bulyanhulu mpaka Bukombe.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tupo katika awamu ya kwanza ya kutekeleza mradi wa gridi imara ambao umeshafikia 42% na tukimaliza tutakuja kwenye awamu ya pili, ambapo na Mbogwe pia, watapata kunufaika na kituo cha kupooza umeme kupitia kile ambacho kitajengwa Bukombe.
Mheshimiwa Spika, swali la pili la maeneo ambayo ameyataja ya Nanda, Lulembela, Lugunga pamoja na Masumbwe; ninafahamu Mheshimiwa Mbunge alishaniambia, kulikuwa na maeneo 13 na tayari maeneo saba tumeshayafanyia kazi kwa kuyawekea transformer ambazo zinafanana na mahitaji ya maeneo husika. Nimhakikishie Mbunge na kata hizi ambazo zimebakia na zenyewe tutazifanyia kazi. Ahsante.
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme wa REA kwa vitongoji ambavyo bado havijapatiwa umeme wa REA Mbogwe?
Supplementary Question 2
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Je, ni lini Serikali itaenda kutoa fedha, kwa ajili ya kumalizia vijiji na vitongoji 188 katika Wilaya ya Nyang’hwale?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, tunayo miradi ambayo inaendelea, ukiwemo Mradi wa Vitongoji 15 kwenye kila Jimbo, ambapo pia na Nyang’hwale inanufaika. Katika mradi huu ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni Nyang’hwale pia, itaendelea kunufaika kwa vitongoji katika jimbo hilo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mkakati wa Serikali upo na tayari unafanya kazi.
Mheshimiwa Spika, mikakati mingine ipo, ikiwemo huu mradi ambao upo sasa hivi unakaribia kuanza. Ahsante.
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme wa REA kwa vitongoji ambavyo bado havijapatiwa umeme wa REA Mbogwe?
Supplementary Question 3
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, je, Serikali mna mpango gani au mkakati gani wa kumaliza kutoa nguzo za miti na kuweka za zege ndani ya Jimbo la Temeke ili umeme usikatikekatike tena?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali upo na unaendelea. Kwa kila mwaka wa fedha tunatenga fedha, kwa ajili ya kufanya miradi hiyo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Temeke tunafanya hivyo, kwa ajili ya ukarabati kuhakikisha tunaendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme. Tunaendelea kufanya hivyo, ili wananchi wa Temeke waendelee kupata umeme wa uhakika.
Name
Bahati Keneth Ndingo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mbarali
Primary Question
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme wa REA kwa vitongoji ambavyo bado havijapatiwa umeme wa REA Mbogwe?
Supplementary Question 4
MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Spika, ni lini sasa mkandarasi wa kupeleka umeme kwenye Vitongoji vya Wilaya ya Mbarali ataripoti? Ninakushukuru.
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ipo mikoa mitatu ambayo tulikuwa hatujapata wakandarasi, ikiwemo Mbeya, Singida na Tanga, lakini tulishapata wakandarasi na wiki hii wataenda kutambulishwa kwa Wakuu wa Mikoa na kukabidhiwa site, ikiwemo Mbeya na hususan kwenye Jimbo la Mbarali la Mheshimiwa Mbunge.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved