Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maimuna Ahmad Pathan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio?

Supplementary Question 1

MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali na kwa Serikali kuwajali watoto wetu, lakini nina ombi moja kwa Serikali. Fedha zilizopelekwa kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule zile ni kidogo sana, na tukiangalia Mkoa wa Lindi ni sehemu hatarishi kwa mara mbili. Hatarishi zingine zilizopo za kawaida, lakini pia kuna hatarishi za wanyama hawa wanaitwa tembo, tembo wanatembea sana usiku kwenye maeneo yale. Nitoe ombi rasmi kwa Serikali kwa Mkoa wa Lindi, kwa shule zilizoko Mkoa wa Lindi, ni hatari sana kwa watoto wetu wanapotoka madarasani usiku na wanapokwenda kupata huduma za kijamii nje, kama kwenda toilet.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Serikali, tufanye mchakato huu kwa haraka kwa sababu shule zile uzio haujakamilika, ili tupate pesa hizo kwa haraka tumalizie uzio ili kuwanusuru watoto wetu, ahsante sana. (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemwelewa Mheshimiwa Mbunge na maombi yake kama Serikali tumeyapokea. Tutaweka kipaumbele katika kuhakikisha kwamba tunajenga uzio katika shule ambazo zipo katika maeneo hatarishi, siyo tu Mkoa wa Lindi, lakini maeneo yote nchini na hasa yale maeneo ambayo yapo karibu na maeneo yenye wanyamapori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari katika Mkoa wa Lindi tumeshaanza kujenga uzio kama nilivyotangulia kusema; Shule ya Sekondari ya Lindi Wasichana imejengewa uzio, Nachingwea Girls imejengewa uzio, Shule ya Msingi ya Namakonde imejengewa uzio na tunaendelea na kazi hiyo kufikia shule nyingine nyingi kuhakikisha na zenyewe zinajengewa uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na mali zao, lakini kwa kuhakikisha tu usalama kwa ujumla wake. Kwa hiyo, tumepokea maombi yako Mheshimiwa Mbunge na tutayafanyia kazi. (Makofi)

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio?

Supplementary Question 2

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Rugambwa Secondary ni shule ya wasichana ya siku nyingi ambayo iko Mkoani Kagera, na kwa kuwa haina uzio shule hii inaweza ikaingiliwa na watu wabaya wakati wowote kutoka pande zote nne.

Je, ni lini Serikali itajenga na kumaliza uzio kuzunguka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inajenga uzio katika shule zetu hizi kwa ajili ya lengo kuu la kuhakikisha usalama wa wanafunzi, lakini mali za shule. Serikali inafanya hivyo kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri, na hivyo naomba nitumie nafasi hii kuwakumbusha Wakurugenzi wa Mamlaka zile za Serikali za Mitaa kuweza kufanya tathmini katika shule ambazo ziko katika mazingira yenye mazingira hatarishi, wafanye tathmini ya gharama zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule hizo na kuweka katika mipango na bajeti ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kuanza kujenga uzio katika shule hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Benardeta Mushashu naomba ukae ukiwa na matarajio kwamba katika Shule hii ya Wasichana ya Rugambwa itajengewa uzio ili kuendelea kuimarisha usalama wa wanafunzi, lakini mali za shule. (Makofi)

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio?

Supplementary Question 3

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwa kuwa maeneo mengi ya shule yanavamiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Je, Serikali haioni sasa umefika wakati muafaka wanapotenga bajeti ya kujenga shule basi wanatenga na bajeti ya uzio ili shule inapokamilika inakuwa imekamilika na uzio wake kuepusha hayo mambo mengine? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, uzio ni sehemu muhimu sana ya miundombinu inayohitajika kwa ajili ya kujenga shule zetu hizi, na ni kweli kabisa Serikali inaweka msisitizo mkubwa.

Kwanza, Serikali inajenga kwa awamu, kwa hiyo, fedha tayari zinatoka kwa ajili ya kujenga miundombinu ya msingi kabisa ambayo itawezesha wanafunzi kupokelewa kwa ajili ya kuanza masomo katika shule hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya majengo haya ya msingi kuwa yamekamilika, ni wajibu wa msingi wa Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa kupitia mapato ya ndani waweze kuhakikisha wanaweka katika bajeti ya mapato ya ndani kujenga uzio. Kwa hiyo, Mheshimiwa Tunza Malapo, Serikali itaendalea na mikakati hii ya kuhakikisha kwamba kupitia fedha za mapato ya ndani ya halmashauri inafika katika shule mbalimbali kwa ajili ya kujenga uzio.

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule za Sekondari za Mwanzi na Shule ya Wasichana ya Solya ambazo zipo Manyoni hazina uzio, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba tunajenga uzio au fence katika shule hizi? Ahsante sana.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia dhana nzima ya ugatuzi wa madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda kwenye Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa, wajibu wa msingi wa kuweza kujenga miundombinu katika shule zetu, lakini katika sekta muhimu kabisa hizi ambazo zinagusa wananchi, ni wajibu wa Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa. Serikali Kuu inaongeza nguvu kuhakikisha kwamba pale ambapo Mamlaka zetu za Serikali za Mtaa zimefika, basi zinaongezewa nguvu katika miradi hii ya maendeleo ikiwemo katika sekta ya elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumkumbusha Mkurugenzi wa Halmashauri hii aweze kufanya tathmini katika shule hizi ambazo amezitaja Mheshimiwa Dkt. Chaya na kubaini bajeti inayohitajika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hii ya uzio katika shule hizi, na aweke katika mipango na bajeti ambayo inatokana na mapato ya ndani kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanajenga uzio katika shule hizi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa wanafunzi, lakini mali za shule. (Makofi)

Name

Amandus Julius Chinguile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nachingwea

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio?

Supplementary Question 5

MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na tunaishukuru Serikali kwa ujenzi wa shule nyingi mpya za msingi na sekondari. Ziko shule ambazo zimejengwa katikati ya makazi ya watu na hii ni kutokana na miundombinu ambayo ilishajaa tangu zamani.

Je, Serikali haioni haja sasa wakati wa ujenzi wa shule hizi ambazo ziko katikati ya makazi ya watu, ni vizuri tukapeleka na component ya uzio ili kuweza kulinda vijana wetu wanaosoma katika maeneo haya? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na Sera ya Elimu Bila Malipo udahili wa wanafunzi umeongezeka maradufu na mazingira hayo yametengeneza uhitaji mkubwa sana wa ongezeko la miundombinu ya shule. Serikali Kuu kwa wakati huu kipaumbele chake namba moja ni kuhakikisha inajenga miundombinu ya msingi kabisa ambayo itawezesha kuanza kupokea wanafunzi hawa waweze kuanza kupata masomo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia na dhana hii ya D by D yaani ugatuzi wa madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda kwenye Mamlaka zile za Serikali za Mitaa, wajibu wa msingi wa kutenga bajeti na kupanga maendeleo ikiwemo kujenga miundombinu ya msingi kabisa katika sekta hizi za elimu, afya na kadhalika, ni wajibu wa Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa, kazi ambayo inafanyika na Serikali Kuu ni kuongeza nguvu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niendelee kutumia nafasi hii kuwasisitiza Wakurugenzi katika Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa waweze kufanya tathmini katika maeneo ambayo yanahitaji uzio katika shule ambazo zinahitaji uzio, lakini siyo tu shule, hata katika vituo vyetu vya kutolea huduma ya afya, wafanye tathmini ya fedha inayohitajika kwa ajili ya kujenga miundombinu hiyo na waweze kuweka katika mipango na bajeti za mapato yao ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kuhakikisha wanaanza kujenga miundombinu hii muhimu kabisa ya uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi au tuseme wananchi kwa upande wa Sekta ya Afya, lakini mali za shule na vituo vya afya.

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio?

Supplementary Question 6

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzio wa waya katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mara iliyoko katika jimbo langu unaonekana kutokutosheleza yale mahitaji yaliyokusudiwa. Je, ni lini sasa Serikali itajenga uzio kwa kutumia matofali ili kutosheleza mahitaji tunayoyataka?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kupongeza jitihada zilizofanyika katika kujenga uzio katika eneo alilolitaja Mheshimiwa Mbunge, na japo Mheshimiwa Mbunge anaeleza kwamba uzio huu haujitoshelezi na kuna uhitaji wa uzio kwa kutumia matofali, naomba nitumie nafasi hii kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri aweze kufanya tathmini kwa kuzingatia maombi aliyoyasema Mheshimiwa Charles Kajege na afahamu kwamba ni kiasi gani cha fedha zinahitajika kwa ajili ya kujenga uzio huu kwa matofali kama alivyoomba Mheshimiwa Mbunge, na aweze kuweka katika mipango na bajeti ya halmashauri, kwa maana ya mapato ya ndani ili hatimaye waje waweze kujenga uzio huu kwa kiwango alichokitaja Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)