Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 1

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, kwanza, naipongeza Serikali kwa majibu mazuri ambayo yanatia matumaini, lakini pili, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru sana Serikali kwanza kwa kutekeleza ahadi yake ya kutupatia gari kwenye kituo changu cha polisi pale Nanyumbu, kwenye Mji wetu wa Mangaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, gari lile ni muhimu sana hasa ukizingatia kwamba sisi watu wa mipakani tunahitaji gari la uhakika kwa shughuli za ulinzi. Nawapongeza sana Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, majibu ya Serikali yanaeleza kwamba kituo hiki cha Polisi kitajengwa kwenye Kitalu F ambapo Halmashauri yetu ya Wilaya ya Nanyumbu imetoa. Hivyo nampongeza sana Mkurugenzi kwa kutoa ardhi hii kwa ajili ya ujenzi huu. Sasa naiomba Serikali inipe commitment, ujenzi huu wa kituo hiki cha polisi Daraja la B, kweli utaanza katika mwaka huo wa fedha ulioutaja?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza, nipokee pongezi alizotoa Mheshimiwa Mbunge. Pongezi ziende kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga fedha kwa ajili ya kazi kubwa ya upatikanaji wa magari kwa ma-OCD wote nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kupitia Jeshi la Polisi imekuwa ikijenga Vituo vya Polisi vya makamanda wa mikoa na wilaya na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Wilaya ya Nanyumbu tunajua iko mpakani na kwa ajili ya usalama wa wananchi wake, nimhakikishie Serikali imeji-commit kwa mwaka wa fedha 2026/2027 tunajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu, ahsante sana. (Makofi)

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 2

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, nimekuwa nikifuatilia kuhusiana na ujenzi wa vituo vya kisasa na vyenye hadhi katika Wilaya za Kipolisi za Kanda Maalum Tarime – Rorya ambazo ni Sirari, Shirati, Nyamwaga, Utegi na Tarime na tunashukuru Tarime mmeanza kujenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini sasa mtajenga vituo hivi vingine vya kipolisi vya hizi wilaya ambazo nimezitaja zilizoko katika Kanda Maalum ya Tarime – Rorya ikiwepo na Bunda? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana,n naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Esther Matiko amekuwa mdau sana wa Wizara ya Mambo ya Ndani, amekuwa akifuatilia ujenzi wa vituo hivi na kama ambavyo tumshajenga Kituo hiki cha Tarime – Rorya, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, vituo hivi vingine alivyovitaja pia tutaviweka kwenye mpango. Hatutajenga mara moja, tutajenga awamu kwa awamu. Serikali inatenga fedha kila mwaka wa fedha. Kwa hiyo, nimhakikishie hivyo alivyovitaja pia tutaweka kwenye mpango tayari kwa kutengewa fedha kwa ajili ya kujengwa, ahsante sana. (Makofi)

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 3

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru, nyumba za askari wetu wa Tabora Mjini zimechakaa na hazifanani kabisa na watu kuishi ndani ya nyumba zile. Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba mpya katika eneo hilo hilo ili askari wetu waweze kuishi kwenye mazingira salama na rafiki kutokana na kazi ambayo wanaifanya? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hawa Mwaifunga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Jeshi la Polisi itafanya tathmini kuona je, kama hizo nyumba zinafaa kwa ukarabati au kujenga upya na baada ya tathmini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba nyumba hizo tunazijenga vizuri ili askari wetu waweze kukaa katika mazingira bora na kufanya kazi, ahsante sana. (Makofi)

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 4

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa vituo vya polisi na makazi ya polisi ni muhimu sana katika kila maeneo, sasa je, ni lini Serikali itakuja na mpango mkakati wa kuainisha vituo vya polisi na makazi ya polisi nchi nzima badala ya kila mtu kuomba kwenye jimbo lake kama hivi ilivyo sasa? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asha Juma kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ina mpango wa kujenga vituo vya polisi kwenye kata zote kwa upande wa Tanzania Bara na shehia kwa upande wa Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba pia na baada ya ujenzi wa vituo hivyo vya polisi, tutatenga fedha pia kwa ajili ya ujenzi sasa wa nyumba za kuishi askari wetu katika maeneo hayo ili watoe huduma kwa wananchi wetu, ahsante sana. (Makofi)

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 5

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona, kwanza, nianze kw akulipongeza Jeshi la Polisi nchini, juzi nilikuwa jimboni Mheshimiwa Naibu Waziri, yakatokea ya kutokea majambazi yakaingia kwenye Mji wa Mbogwe na wakakabiliana nayo na wakamaliza vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto walizonazo Mbogwe, askari hawana nyumba za kuishi, lakini pia kituo hawana. Mimi nilishachukua tayari eneo la kujenga kituo cha polisi.

Sasa swali langu la msingi, ni lini Mheshimiwa Waziri utatoa pesa ili kusudi Wilaya ya Mbogwe kituo kijengwe, lakini pia na gari wapate ili waendelee kukabiliana na majambazi? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nicodemas Maganga, Mbunge wa Mbogwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tunalipongeza jeshi letu kwa kweli kwa kazi kubwa linayofanya ya kulinda raia na mali zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ameshatenga kwa halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi kwa maana eneo la Mbogwe. Nimhakikishe tutaliingiza kwenye mpango ili tutengee fedha sasa upande wa Serikali ili tuweze kujenga kituo hicho cha polisi ambacho kitasaidia usalama wa raia na mali zao katika eneo la Mbogwe, ahsante sana. (Makofi)

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 6

MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba uniruhusu nimpongeze kwa dhati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mheshimiwa Bashungwa pamoja na Mheshimiwa Sillo kwa kusikia kilio cha wananchi wa Wilaya ya Micheweni kuhusu ujenzi wa Kituo kipya cha Wilaya ya Micheweni. Hivi ninavyokwambia tayari ujenzi umeanza.

Sasa naomba niulize, ni lini Serikali itawajengea polisi wetu wa Wilaya ya Micheweni makazi ya kudumu? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Omar Kombo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kumaliza ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Micheweni, sasa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha sasa tunajenga nyumba za askari wetu katika eneo hilo, ahsante.

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 7

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, mwaka 2021 tulianza ujenzi wa kituo cha polisi pale Kishapu na kwa bahati nzuri tumefikia hatua nzuri, shilingi milioni 100 zimetumika katika hatua ya upauaji ambayo tumeifikia kwa sasa. Hii ni nguvu za wananchi, Mfuko wa Jimbo pamoja na Mgodi wa Mwadui ambao umechangia fedha kwa ajili ya ujenzi huu. Sasa Serikali iliweka kwenye mpango wa mwaka huu ambao tunaumalizia kwamba ingetekeleza kwa ku-support hizi nguvu zote kwa ajili ya kukamilisha mradi huu.

Je, Serikali sasa iko tayari kukamilisha mradi huu ili mradi adha tuliyonayo pale tuweze kuondokana nayo? (Makofi)

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Butondo, Mbunge wa Kishapu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge, yeye mwenyewe kama Mwenyekiti wa Mfuko wa Jimbo kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki, wananchi wake wa Kishapu pamoja na mdau ambaye ni Mgodi wa Almasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu imekuwa ikiunga mkono juhudi kama hizi ambazo wananchi wameji-commit na nimhakikihsie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari kwa sababu tumeshaongea na Mheshimiwa Mbunge kwenye mwaka wa fedha sasa unaoanza 2025/2026 tunatenga fedha kwa ajili ya kumalizia Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kishapu, ahsante sana. (Makofi)

Name

Issa Jumanne Mtemvu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 8

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Jimbo la Kibamba tunatoa shukrani sana kwa Serikali kupitia Kituo chetu cha Polisi cha Wilaya ya Chagogoni, kinaendelea kufanya kazi vizuri sana, lakini ni ukweli Jimbo la Kibamba liko pembezoni sana mwa Dar es Salaam na lina idadi kubwa sana ya watu. Sasa eneo la kusini ambao ni King’azi A, King’azi B, Mpakani, Kwa Unju, Saranga na Mtaa wa Ukombozi, ina zaidi ya watu 300,000 na hamna kituo chochote cha polisi cha kuwasaidia usalama nae neo tayari wanalo.
Je, Serikali mnaweza mkaweka commitment ya kutusaidia pale kwa ujenzi wa haraka ili wananchi wapate usalama wao? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Issa Mtemvu, Mbunge wa Kibamba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu tayari wameshatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi. Sisi kama Serikali tunachuku eneo hilo, tunaliingiza kwenye mpango na tayari kwa kutengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi kwenye eneo ambalo lina watu zaidi ya 300,000 kwa ajili ya usalama wao na mali zao, ahsante sana.

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 9

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nyumba za askari polisi katika Jimbo la Muhambwe ni chakavu sana.

Je, ni lini Serikali itajenga au kukarabati zile nyumba ambazo ni chakavu sana ili kuweka mazingira safi kwa askari wetu wa Jimbo la Muhambwe? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Samizi, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Jeshi la Polisi itafanya tathmini katika maeneo yote ikiwemo na Wilaya ya Muhambwe ili kuona kwamba je, nyumba hizo zinafaa kujengwa au kukarabatiwa. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nyumba zako za askari katika eneo la Muhambwe pia tutalichukua, tutafanya tathmini na kuingiza kwenye mpango tayari kwa ajili ya ukarabati au ujenzi kutokana na hali tutakayoikuta, ahsante sana. (Makofi)

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Supplementary Question 10


MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Ifikapo tarehe 15 mwezi ujao, Wilaya ya Liwale inafikisha miaka 50 lakini haijawahi kuwa na jengo la kituo cha polisi. Ni nini mpango wa Serikali kujenga kituo cha polisi ili wananchi wale wasiendelee kupanga? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer


NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zuberi Kuchauka ambaye swali hili ameshauliza mara nyingi na nimeshamjibu, lakini nimhakikishie Serikali hii sikivu ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inajua ukosefu wa kutokuwa na kituo cha polisi katika Wilaya ya Liwale na iko tayari imeshawekwa kwenye mpango na itatengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ili kuhudumia wananchi na mali zao, ahsante sana. (Makofi)