Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Makao Makuu ya TANAPA katika Halmashauri ya Mji wa Bunda?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Bunda TC ilitenga eneo hilo kwa kutumia hela milioni 85 kuwalipa watu fidia na ikawapa Kanda ya Magharibi ya TANAPA bure wajenge, toka 2014 mpaka leo ni kama miaka mitano iliyopita. Swali la kwanza; je ni lini sasa Serikali itaamua kwa maksudi kujenga eneo hilo ambalo watu wa Bunda wanalihitaji?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Wilaya ya Bunda na Wilaya ya Butiama ili waende kwenye Hifadhi ya Serengeti inabidi waende Serengeti Wilayani au waende Lamadi. Sisi tuna geti la kutoka Kata ya Mgeta kwenda Kilawila kilometa 17. Je, ni lini Serikali au TANAPA itafungua geti hilo kwa watu wa Bunda? ninakushukuru.
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi kazi ya ujenzi itaanza mwaka wa fedha 2025/2026. Kuhusiana na swali lake la pili la kufungua geti hilo, kwa sasa kuna mageti ambayo yanafanyiwa kazi tukimaliza kukamilisha mageti haya tutaweka kwenye mpango unaofuata kulingana na vipaumbele vya ufunguaji wa hifadhi za Taifa.
Name
Noah Lemburis Saputi Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Makao Makuu ya TANAPA katika Halmashauri ya Mji wa Bunda?
Supplementary Question 2
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi. Ninataka kufahamu kwa kuwa wanyamapori wanawasumbia wananchi kwenye Vijiji vya Oljorobusi na Engaraoni na nilishawasilisha kwako kwa Naibu Waziri akatoa majibu kituo cha dharura kijengwe katika vijiji hivyo na hadi sasa kituo hicho cha dharura hakijajengwa. Je, nini kauli ya Serikali ili kuwanusuru wananchi ambao wanasumbuliwa na wanyama hasa tembo?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali lanyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya wanyama wakali na waharibifu na ndiyo maana inatumia mikakati mbalimbali kuhakikisha inawadhibiti, sasa tumeingia kwenye matumizi ya teknolojia ya ndege nyuki, vilevile maeneo mengine tunatumia helkopta na tunatumia vilevile matumizi ya mabomu baridi.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuhusu ujenzi wa vituo tunaendelea nalo kwa jinsi ambavyo upatikanaji wa fedha unapatikana. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na subira bado nia ya serikali ni kujenga kituo kwenye eneo lile.
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Makao Makuu ya TANAPA katika Halmashauri ya Mji wa Bunda?
Supplementary Question 3
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Hifadhi ya Mwalimu Nyerere pamoja na pori la akiba la Selous Game Reserve linapakana na Liwale. Je, Serikali haioni imefika wakati sasa kujenga geti la kuingilia watalii Wilayani Liwale ili wana Liwale nao wafaidi faida za utalii kwenye nchi hii? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo mipango ya kujenga mageti kwenye maeneo mengi na kwa upande huu wa Mikoa ya Kusini tunao mkakati madhubuti wa kuifungua Mikoa hii ya Kusini kwenye suala la utalii. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira tumalizie kazi ambazo tunazifanya sasa hivi tukikamilisha tutahamia kwenye maeneo yake.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved