Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Daimu Iddi Mpakate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga maghala ya kuhifadhia mazao Vijijini?
Supplementary Question 1
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa tatizo la maghala kwenye vyama vya msingi na vijiji vyetu katika Jimbo la Tunduru Kusini ni kubwa. Ni kwa nini sasa Serikali haioni haja ya kuwashirikisha benki za biashara na vyama vya msingi katika kujenga maghala ili kuondokana na adha ya vyama vya msingi kutumia nyumba za watu binafsi ambazo hazina ubora wa kuhifadhia mazao?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; mwaka wa fedha 2014/2015 Bodi ya Korosho ilianza kujenga ghala la kuhifadhia mazao katika Mji wa Tunduru lenye uwezo wa kuhifadhi mazao tani 10,000, lakini ujenzi ule umesimama mpaka leo. Je, ni lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi ule kwa kuwa bilioni moja iko pale na bado haifanyi kazi yoyote?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mpakate kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo lake hususani kufuatilia maghala ya uhifadhi wa chakula. Ninamthibitishia tu kwamba mpango wa Serikali wa sasa tumevielekeza vyama vya ushirika na vile vyama vya msingi na vyama vikuu pamoja na sekta binafsi kuingia katika ujenzi wa maghala ambayo yatasaidia katika uhifadhi wa chakula. Kwa hiyo, jambo hili lipo katika mpango wetu na tumeendelea kulisukuma kwa sasa hivi.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili ambalo ni la msingi kabisa ni kwamba ni kweli Bodi ya Korosho ilianza kujenga katika Mwaka wa Fedha 2014/2015 na hapo Katikati tulikwama kupata fedha, lakini ninavyozungumza sasa hivi ni kwamba tayari Bodi ya Korosho ina fedha bilioni 2.6 kwa ajili ya ujenzi wa ghala hili. Tumeshawalekeza kwamba katika msimu unaofuatia ghala lile liwe limejengwa limekamilika na lianze kutumika kwa ajili ya kuhifadhia mazao. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved