Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza:- Je, Serikali imefikia wapi katika mpango wa ujenzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mwalimu Nyerere pamoja na hosteli Pemba?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake, lakini ninaomba nipate ufafanuzi. Swali la kwanza; huo utekelezaji wa hayo mafunzo upoje na umeanza vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Serikali haioni haja sasa ya kutoa orodha yote ya hivi vyuo vikuu vipya ilivyovianzisha ili tujue vimefikia kiwango gani cha utekelezaji? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba Serikali tayari imefanya ujenzi na baadhi ya majengo yamekamilika na mengine yanaendelea kukamilika. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeanza kutoa mafunzo katika chuo hiki katika Kampasi yetu ya Pemba na mpaka tunavyozungumza sasa hivi kuna jumla ya wanafunzi 218 kwa mgawanyo ufuatao:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi 218 ni wa astashahada; 145 ni wa stashahada; na 30 ni wa shahada. Aidha, wahadhiri waliokuwepo katika kampasi ile ni 24 na watumishi wa kawaida ni 14. Kwa hiyo, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ipo kazini nimwondoe wasiwasi na kazi kule inaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu orodha, ninaomba Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu liridhie kwamba tuandae orodha hii na miradi hii ya vyuo vikuu katika maeneo yote inakotekelezwa na kujua status yake katika kila eneo kuna asilimia ngapi za utekelezaji katika ujenzi wa miradi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana.