Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itazipatia fedha za ukarabati Shule Kongwe za Msingi Makanya na Kwai katika Jimbo la Lushoto?
Supplementary Question 1
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru na ninaishukuru Serikali nimeona kweli fedha zile zimefika na kazi imeshaanza.
Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili; Shule za Msingi Kwemashai, Mshezee, Chumbageni, Mazumbai na Mkuzi nazo zimechakaa mno. Je, Serikali haioni sasa kuna ulazima wa kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kukarabati shule hizi kwa pamoja? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali haioni kwamba kuna lazima sasa za kujenga nyumba za walimu ili kuondoa changamoto zetu za walimu hawa kwa ajili ya kukaa karibu na vituo yao vya kazi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ni kweli kwamba shule ambazo Mheshimiwa Shekilindi amezitaja, Shule ya Chumbageni, Kweshai na nyingine ambazo amezitaja ni shule kongwe na chakavu ambazo zinahitaji kufanyiwa ukarabati, lakini pia ujenzi wa miundombinu mingine mipya. Ninaomba nimuhkikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba moja ya vipaumbele vya Serikali kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Shule za Msingi (BOOST) ni kuendelea kuzitambua kwanza shule chakavu, lakini pia kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati. Shule hizo tayari tumezitambua na tumeziingiza kwenye mpango wa kwenda kuzikarabati kwa awamu.
Mheshimiwa Spika, suala la pili kuhusiana na ujenzi wa nyumba za walimu; katika bajeti zetu kuanzia mwaka 2020/2021 mpaka sasa na hata bajeti ya mwaka ujao 2025/2026, Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuendelea kujenga nyumba za walimu kwa awamu, ili kuwawezesha walimu wetu kuishi mazingira bora na pia kuwa karibu na shule ambazo wanafundisha. (Makofi)
Name
Anna Richard Lupembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itazipatia fedha za ukarabati Shule Kongwe za Msingi Makanya na Kwai katika Jimbo la Lushoto?
Supplementary Question 2
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni lini Shule ya Tambazi, Kata ya Katumba itafanyiwa marekebisho kwa sababu imechakaa sana na ni shule kongwe? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimuhkikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutafuatilia kupata taarifa za Shule hiyo ya Msingi Tambazi na kuona gharama za fedha ambazo zinahitajika kwa ajili ya ukarabati. Nitumie nafasi hii kumuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kufanya tathmini kupitia Engineer wa Halmashauri na kutuletea taarifa za mahitaji ya fedha, ili tutenge fedha either kutoka mapato ya ndani kwa awamu pia kutoka Serikali Kuu. (Makofi)
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itazipatia fedha za ukarabati Shule Kongwe za Msingi Makanya na Kwai katika Jimbo la Lushoto?
Supplementary Question 3
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kunipatia nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuendelea kuleta fedha kujenga shule shikizi kwenye maeneo ambayo watoto wanasoma maeneo ya mbali, kwa mfano, Kata ya Kerege na Mapinga, Vitongoji vya Kimere na Amani? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka kipaumbele cha hali ya juu katika kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi zikiwemo shule na katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 mpaka sasa Serikali imeendelea kutenga fedha na kujenga shule shikizi katika maeneo ambayo yanahitaji kujengwa shule hizo.
Kwa hiyo, ninaomba nimuhakikishie Mheshimiwa Subira Mgalu kwamba tutakwenda kuanza ujenzi wa shule katika maeneo hayo ikiwa yatakidhi vigezo, kwa maana idadi ya wanafunzi watarajiwa katika eneo husika na pia ukubwa wa vitongoji au vijiji hivyo ili wananchi hao na watoto waweze kusoma karibu zaidi.
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itazipatia fedha za ukarabati Shule Kongwe za Msingi Makanya na Kwai katika Jimbo la Lushoto?
Supplementary Question 4
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, ahsante, je, ni lini Serikali itakarabati Shule ya Msingi Kitingi na Shule ya Msingi Lusimbi katika Kata ya Kwa Kivu? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali ilishaainisha shule zote kongwe na chakavu, lakini pia kuanza kufanya tathmini ya uhitaji wa fedha kwa ajili ya ukarabati kwa awamu.
Kwa hiyo, ninaomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaendelea kutenga fedha kwenye bajeti zetu kupitia mapato ya ndani na pia kupitia Serikali Kuu kwa ajili ya kuanza ukarabati wa shule hizo kongwe ambazo ni chakavu katika jimbo hilo.
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itazipatia fedha za ukarabati Shule Kongwe za Msingi Makanya na Kwai katika Jimbo la Lushoto?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, Shule ya Msingi Kilima A iliyopo Nyohogo, Wilaya ya Kahama imechakaa sana, je, nini mpango wa Serikali kukarabati shule hiyo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ninaomba nitumie nafasi hii kwanza nimkumbushe Mkurugenzi wa Halmashauri husika kwamba wanawajibika kutuletea taarifa rasmi za tathmini za mahitaji ya ukarabati wa shule hiyo na nimuhakikishie Mheshimiwa Dkt. Christina kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI tutakwenda kufuatilia na kuona shule hiyo inahitaji kiasi gani cha fedha ili tuanze kutenga fedha kwa ajili ya kuikarabati shuke hiyo. (Makofi)
Name
Sylivia Francis Sigula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itazipatia fedha za ukarabati Shule Kongwe za Msingi Makanya na Kwai katika Jimbo la Lushoto?
Supplementary Question 6
MHE. SYLIVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Shule ya Msingi Ilemba ni ya mwaka 1973 imechakaa sana na madarasa hayatumiki kwa usalama wa wanafunzi. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha za kukarabati shule hiyo? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule chakavu sana za msingi na Serikali ambazo zinahitaji ukarabati kwa haraka. Kwa hiyo, ninaomba nimuhakikishie Mheshimiwa Sylivia kwamba tutakwenda kufuatilia na kuona uhitaji wa gharama za ukarabati, ili tuanze kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukarabati shule hiyo. (Makofi)