Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amb. Liberata Rutageruka Mulamula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Primary Question

MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya kimkakati ya Kyazi Kayanga – Missenyi?

Supplementary Question 1

MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kipindi hiki na kuharibu barabara nyingi pamoja na hiyo barabara ya kimkakati aliyoitaja Mheshimiwa Waziri; je, mkandarasi atawezeshwa kujenga makalavati na madaraja yale madogo madogo ambayo yameharibiwa na mvua hii kubwa? Maana yake madaraja mengi yameondoka kwenye hiyo barabara. Ninakushukuru. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ni kweli kwamba katika msimu uliopita tulipata mvua nyingi na zilileta athari kwenye barabara mbalimbali ikiwemo barabara hii ambayo ipo katika Jimbo la Missenyi, Barabara ya Kyazi Kayanga – Missenyi na ndio maana katika bajeti ya mwaka ujao tumeitengea bajeti ya shilingi milioni 59 kwa ajili ya marekebisho katika maeneo korofi. Pia Serikali itaendelea kuona maeneo ambayo yanahitaji ujenzi wa makalavati na madaraja kwa udharura Serikali itaendelea kutumia fungu lake la dharura kwa ajili ya kurekebisha barabara hiyo, ili iweze kupitika vizuri. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaifanyia kazi. (Makofi)

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya kimkakati ya Kyazi Kayanga – Missenyi?

Supplementary Question 2

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Migombani kata ya Nitekela kipo kisiwani kwa sababu barabara zote ambazo zinaingia kijijini hapo zimekatika kwa sababu ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha Mkoani Mtwara. Je, Serikali ina mpango gani wa dharura kuhakikisha kwamba, wanarejesha mawasiliano katika kijiji hiki? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Kijiji hicho cha Migombani katika Jimbo la Nanyumbu kilipata athari pia na mvua barabara nyingi zilikatika na kufanya kufikika kijiji hicho kuwa na changamoto. Tayari kupitia Meneja wa TARURA wa Nanyumbu na Mkoa wa Mtwara, Ofisi ya Rais, TAMISEMI - TARURA tumeshakubaliana kwamba, tutapeleka fedha mapema iwezekanavyo kwa sababu tumeshafanya tathmini ya mahitaji ya fedha kwa ajili ya kwenda kukarabati.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Chikota kwamba ni suala tu la muda Serikali itakwenda kurejesha miundombinu hiyo katika Kijiji jhicho. (Makofi)

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya kimkakati ya Kyazi Kayanga – Missenyi?

Supplementary Question 3

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, ahsante, fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha kimkakati katika Jimbo la Mwibara bado hazijafika. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha hizo? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali ilitenga shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kupeleka fedha kwenye vituo vya afya vya kimkakati kwenye majimbo 120 awali na mpaka sasa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwishatoa bilioni hizo 30 na majimbo yetu yameanza kupokea fedha hizo zaidi ya 80% na 90%. Nikuhakikishie tu Mheshimiwa Kajege pia katika Jimbo la Mwibara taratibu za kupeleka fedha zinafanyika na ninaamini ndani ya wiki hii kwenye kile kituo cha afya ambacho ulikiweka kama cha kimkakati kwa kila jimbo fedha itaingia katika jimbo hilo. (Makofi)