Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, nini sababu ya Wilaya ya Nkasi kukosa miradi ya kimkakati?
Supplementary Question 1
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru na nimeyasikia majibu ya Serikali. Kwa kuwa mahitaji ya Wilaya ya Nkasi ni soko pamoja na stendi na kwa mujibu wa wataalam suala la soko hati tumepata na stendi. Gharama za kujenga soko ni shilingi bilioni 1.3. gharama ya kujenga stendi ni shilingi bilioni mbili. Serikali mpo tayari kutujengea miradi hiyo kwa sababu vigezo hivyo vingine vimekamilika?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; hamuoni kuna haja sasa ya kuwajengea uwezo Maafisa Mipango nchi nzima yaweze kuibua miradi ya kimkakati?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza niwapongeze watendaji na viongozi wote wa Halmashauri ya Nkasi pamoja na Mheshimiwa Mbunge kwa kusimamia suala hili ambalo alipewa maelekezo na Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuhakikisha kwamba wanapata hati pia kukidhi vigezo vya mahitaji ya miradi ya kimkakati.
Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, kwa kuwa taarifa ya Mheshimiwa Mbunge kwamba stendi na soko tumeshapata hati na gharama zinazotatarijiwa kufanyika kwa maana ya kutumika kujenga, ninaomba nitumie nafasi hii nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutafutilia ili kupata taarifa rasmi kutoka kwa Mkurugenzi kupitia Katibu Tawala Mkoa na kuja Ofisi ya Rais, TAMISEMI, ili tutenge fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo ya kimkakati kwa awamu.
Mheshimiwa Spika, suala la pili Serikali imekuwa ikifanya mafunzo ya mara kwa mara kwa Maafisa Mipango ili kuwajengea uwezo zaidi wa kuandika miradi ya kimkakati kulingana na mazingira yao. Suala hili Mheshimiwa Mbunge tumepokea ushauri huo tutaendelea kuboresha mafunzo hayo ili Maafisa Mipango wawe competent zaidi katika uandishi wa miradi ya kimakati.
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, nini sababu ya Wilaya ya Nkasi kukosa miradi ya kimkakati?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi hii, mwaka 2023 tuliwasilisha andiko na michoro kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa eneo la Madila; je, mradi huu ni lini utaanza kutekelezwa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, zipo halmashauri kadhaa ikiwepo Halmashauri ya Meru ambayo waliandika miradi ya kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa soko na Serikali imeweka utaratibu; kwanza, miradi inawasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, inafanyiwa uchambuzi wa kukidhi vigezo na baadaye tunawasiliana na Wizara ya Fedha kwa ajili ya kuangalia kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa dkt. Pallangyo tutaendelea kufuatilia kuona andiko hilo limefikia hatua gani, ili baada ya hapo tuone uwezekano kama linakidhi vigezo, uwezekano wa kuanza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi.
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, nini sababu ya Wilaya ya Nkasi kukosa miradi ya kimkakati?
Supplementary Question 3
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilishawasilisha wasilisho la ujenzi wa stendi. Ninataka kujua ni lini sasa Serikali itatoa fedha ili tufanye ujenzi huu? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, tutafanya tathmini ya andiko ambalo limewasilishwa na Halmashauri ya Chemba na baada ya kuona kama linakidhi vigezo basi tutaanza utaratibu wa kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, nini sababu ya Wilaya ya Nkasi kukosa miradi ya kimkakati?
Supplementary Question 4
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante, Halmsahauri ya Wilaya ya Hai iliwasilisha andiko lao la mradi wa kimakakti wa machinjio ya kisasa Kata ya KIA. Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Saashisha Mafuwe kwamba tunafahamu wana mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa, lakini ninafahamu Mheshimiwa Mbunge pia amefuatilia mara kwa mara na tulikubaliana kwamba tunafanya tathmini ya kukidhi vigezo pia tunaangalia uwezekano wa kupata fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wake.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved