Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka fedha za ujenzi wa majengo mapya ya Kituo cha Afya cha Kamsamba – Momba?
Supplementary Question 1
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini specifically kwa hiki kituo alichotaja Mheshimiwa; ni lini hasa baada ya huo je, ni lini? swali la kwanza.
Swali la pili, ni lini Serikali itapeleka vifaatiba katika hospitali mpya ya Uru Kusini? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kama ambavyo nimeanza kujibu katika jibu langu la msingi kwamba Serikali imeweka vipaumbele, tunafahamu mahitaji ni makubwa na tungetamani mahitaji yote yafanyiwe kazi siku moja, vituo vya afya vyote vikarabatiwe, zahanati kongwe, hospitali kongwe, lakini kupanga ni kuchagua kutokana na vyanzo vya fedha. Tumekubaliana tukarabati kwanza hospitali chakavu na kongwe za halmashauri kwa sababu hizi ni hospitali za rufaa ambazo zinatoa huduma kubwa zaidi ndani ya halmashauri, lakini baadaye tutakwenda kwenye ukarabati wa vituo vya afya kongwe na tayari tumekwisha viainisha vituo 203 kikiwemo Kituo cha Afya cha Kamsamba.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimuhakikishie Mheshimiwa Mama yangu Mama Shally Raymond kwamba suala hilo tumelipa kipaumbele na tunatarajia hospitali za halmashauri zitakarabatiwa ndani ya miaka miwili ya fedha na baadaye tutakwenda kwenye vituo vile vya afya.
Mheshimiwa Spika, swali la pili Serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba na katika kipindi hiki cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, vifaatiba vimenunuliwa kwa wingi na kupelekwa kwenye vituo vyote vipya na hospitali zote za halmashauri zilizokamilika lakini na hospitali zile za zamani na mpaka sasa katika mwaka huu wa fedha jumla ya shilingi bilioni 63.7 zimetengwa kwa ajili ya vifaatiba.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutapeleka pia fedha katika Hospitali ya Halmashauri ya Uru Kusini ambayo nina uhakika tayari wamepokea fedha zaidi ya shilingi milioni 900 lakini tunaendelea kupeleka fedha kwa awamu kuhakikisha kwamba vituo hivyo vinakuwa na vifaa tiba vya kutosha. (Makofi)
Name
Tecla Mohamedi Ungele
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka fedha za ujenzi wa majengo mapya ya Kituo cha Afya cha Kamsamba – Momba?
Supplementary Question 2
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Ngunichile ambacho ni cha kimkakati, lakini pia ni ahadi ya viongozi wa kitaifa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, Mama Tecla Ungele, kwamba tunafahamu kwamba kituo hicho ni ahadi ya viongozi wa kitaifa na sisi katika mipango yetu ya utekelezaji ahadi za viongozi wa kitaifa ni kipaumbele nambari moja na tumekwisha ainisha na tayari fedha zimeanza kupelekwa kwenye vituo mbalimbali ambavyo ni ahadi za viongozi wa kitaifa.
Kwa hiyo, naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba tutaendelea kutoa kipaumbele na tutapeleka fedha kwa ajili ya kujenga kituo hiko cha afya cha kimkakati. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved