Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y. MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: - Je, kwa nini Serikali isiagize CAG akague URA SACCOS ya Jeshi la Polisi?

Supplementary Question 1

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, pamoja na majibu ya Serikali lakini bado kumekuwa na malalamiko kuhusiana na hizi SACCOSS ambazo kwenye Idara ya Polisi, lakini na Idara nyingine ambazo zipo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Sasa Serikali mnachukua hatua gani kuhakikisha kwamba mnatekeleza yale madhaifu ambayo mnakuta yametokana na ukaguzi wa CAG? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi SACCOSS hii haikaguliwi na CAG, inakaguliwa kwa mujibu wa sheria namba sita inayosimamiwa na kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika na. 6 ya mwaka 2013 na kama nilivyosema URA SACCOSS hii ni SACCOSS bora hapa nchini kama nilivyosema imepata tuzo toka mwaka 2021/2024 kwa hiyo ni SACCOSS ambayo haina malengo yoyote ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi, ahsante sana.