Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la polisi na gari la zimamoto katika Wilaya ya Kyerwa inayopakana na nchi mbili ili kukabiliana na majanga ya moto?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru Serikali kwa gari ambalo wamepeleka Kyerwa, Wilaya ya Kyerwa ni wilaya changam hatuna kituo cha polisi. Polisi wanafanya kazi kwenye mazingira magumu, kwenye vibanda ambavyo vilikuwa ni vya wakimbizi.

Je, Serikali ipo tayari kuunga mkono juhudi za wadau ambao tayari wameshaanzisha ujenzi wa kituo cha polisi? (Makofi)

Swali la pili, polisi hawana nyumba pale Kyerwa, je, Serikali ipo tayari angalau kwa kuanzia nyumba ya OCD pamoja na OC-CID? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge wa Kyerwa, amekuwa akifuatilia sana kituo cha polisi pamoja na vitendea kazi katika wilaya hiyo. Naomba nijibu maswali ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza niwapongeze wadau ambao tayari walishaanza ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kyerwa ambayo ni wilaya mpya na nimhakikishie Serikali imekuwa ikiunga mkono juhudi za wananchi au wadau wanaofanya kazi hii. Kwa hiyo Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kyerwa pia tutaweka kwenye mpango na kutengewa fedha ili tuweze kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na wananchi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusu nyumba za makazi ni kweli wilaya hii ni mpya, haina nyumba ya OCD wala OC-CID, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tumechukua hili pia tutaweka kwenye mpango tayari kwa kutengewa bajeti kwa ajili ya kujenga nyumba za viongozi hawa wa Polisi wa Wilaya hii ya Kyerwa, ahsante.